Ni Kidijitali Zaidi, Infinix Note 30 Yaja Kuipaisha Infinix
Dar-es-Salaam Juni 5,2023: Infinix Tanzania yazindua matoleo mapya katika series ya NOTE 30,uzinduzi wa Infinix NOTE 30, NOTE 30 PRO na NOTE 30 VIP ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki, Infinix imeweka rekodi mpya ya uchezaji games na utendakazi kwa ufanisi kupitia matoleo hayo. Kwa kichakataji chake cha Dimensity 8050 5G, NOTE 30 Vip 5G ina matumizi bora ya nishati, ikiruhusu kasi ya kuchakata haraka na kufanya kazi nyingi kwa urahisi zaidi. Zaidi ya hayo, Chaji ya Haraka ya (All-Round Fast Charge) 68W na chaji isiyotumia waya ya(wireless charge) 50W huhakikisha kwamba watumiaji wanaweza kuchaji simu haraka wanapocheza bila wasiwasi wa kuongezeka kwa joto. NOTE 30 Vip 5G pia ina onyesho(refresh rate) maridadi la 120Hz FHD+ na kamera yenye nguvu ya 108MP iliyo na vipengele vilivyoboreshwa kwa matumizi mazuri ya upigaji picha.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi Bw.Francis Tu alisema, “Infinix ni brand inayotambulika duniani kote, leo tuna furaha kutangaza Infinix NOTE 30 Series, tumebuni series hii ya NOTE kwa lengo la kuwapa watumiaji simu yenye nguvu inayoweza kuwafanya waunganishwe na ulimwengu, wakati wowote na mahali popote. Ili kufanikisha hili, tulitengeneza suluhisho la kwanza kwa kuvumbua teknolojia ya ‘All-Round Fast Charge’, ambalo sio tu linatoa kasi lakini pia huhakikisha usalama, umaridadi na umahiri. Kwa suluhisho hili, watumiaji wanaweza kudhibiti maisha yao katika hali zote, 24/7. Vifaa vyote vina onyesho bora zaidi, kamera iliyo wazi kabisa, mfumo wa sauti uliosanifiwa na JBL na uwezo wa hali ya juu wa muunganisho. Tuna uhakika kwamba matoleo ya NOTE 30 ni chaguo bora kwa watumiaji wenye kutumia simu zao kama kitenda kazi kikubwa katika pirikapirika za kila siku.”
Afisa Mahusiano wa Infinix, Bi Aisha Karupa wakati akizungumza na waandishi wa habari aliongeza kuwa “Infinix, inaamini kwa dhati kuwa kila mtu anastahili kupata simu janja yenye ubora huku ikikumbukwa kuwa sio kila mtu anaweza kumudu kununua kwa kulipia bei yote kwa simu kama hizi zenye viwango vya hali, kutokana na hilo Infinix imeshirikiana na EasyBuy Tanzania kuhakikisha kuwa wateja wetu wanaweza kununua kwa mkopo pasipo na Riba ili hali mteja inampasa kumaliza denikwa muda wa miezi mitatu, ofa hii ni kwa wateja watakaofanya manunuzi kwa njia ya mkopo kuanzia June 2 hadi July 2”.
Msanii mahiri wa Bongo flavour Mario ambaye pia ni balozi wa Infinix NOTE 30 aliongelea uzoefu aliokuwa nao juu ya bidhaa hii, “Ninahisi kuunganishwa na hii simu nikiwa kama kijana mwenye kazi nyingi za kufanya pasipo kupoteza muda, Infinix NOTE Series imekuwa suluhisho kwangu kwa pande zote, fikiria inachukua dakika 30 tu nishati ya betri kufikia 80%, lakini pia inaniruhusu kucheza michezo wakati simu ikiendelea kujaa chaji, kuchajisha simu nyengine, licha ya kuwa na sifa hizi zotezaidi ninavutiwa na gharama yake ni rahisi kila kijana anaweza kukifikia na kutimiza malengo yake kupitia teknolojia”.
Lakini pia Mario amewataka vijana kukaa karibu na social media page za @infinixmobiletz,kampuni inayomjali na kumthamini kijana mwenye kipaji hivyo kumeandaliwa shindano la Star Alliance ambalo linatarajiwa kuanza hivi punde ni wakati wako kijana kutoboa kupitia kipaji chako. Hafla hiyo ilifanyika Serena Hotel hoteli ya hadhi ya nyota 5 na kuhudhuriwa na wafanyabiashara wa simu, wafanyakazi wa kampuni za mitandao ya simu, Balozi wa NOTE 30 Bwana Mario, wateja wa simu za Infinix na medias mbalimbali.
Zawadi mbalimbali zikiwamo NOTE 30 ziligawiwa kwa maduka bora na wageni waalikwa walioshinda bahati nasibu. Infinix NOTE 30 zinapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania, au piga 0745170222 kwa huduma ya haraka.