The House of Favourite Newspapers

Ni Kweli Mo Dewji Anapata Hasara Simba? JIBU KAMILI HILI HAPA.

0


Kwenye boti la Tajiri MO Dewji tutapanda watu wachache sana waliosikiliza Interview nzima na kumuelewa nini anamaanisha.

Tajiri ambaye anamiliki Makampuni yalioajiri Watanzania zaidi ya 47,000 akiwa ni muajiri wa pili nyuma ya serikali kwa kuajiri watu wengi unahisi anaweza kuongea kitu ambacho hakimake sense??

Wengine wanasema MO hana pesa ama anatoa kwa kinyongo lakini ni MO huyu ambaye amesaini Pledge ya Mabilionea duniani wapo 120 tu ambao wakiwa hai wanatoa sehemu ya Utajiri wao kwa Jamii ku-solve matatizo mbalimbali, ni MO huyu ambaye amesaini pledge kuwa akifa basi 50% ya Utajiri wake wagaiwe kwa mifuko ya hisani, mbona hatumsikii akilalamika huko?

Kwenye mpira wa miguu ni ukweli mchungu kuwa Simba ni HASARA kwake!
Tujiulize anatoa Pesa za usajili wa Wachezaji wa Kimataifa, wanaolipiwa nauli za kuja, malazi, usafiri, agent fee, vibali vya kazi, mishahara na bonus halafu WANAFELI, wanavunjiwa mikataba wanaondoka, Mlipaji ni MO!
Mzigo wote kwake, hapo kuna faida ama hasara?

Team hii inaenda Camp nchi mbalimbali, kwa Wanawake na Wanaume, kuna projects za vijana, gharama za usafiri wa ndege, bonus, kila kitu akaunti za klabu peke yake haziwezi kutoboa! Nani anayetoa mzigo? Jibu ni Mwekezaji, ni nani? Ni MO Dewji, ndio maana anasema kwa mwaka anaingia hasara ya Dola Million 4! Its true hesabu zinapigika na zinaeleweka.

Mmesahau hapa kasajiliwa Aubin Kramo ni majeruhi, kosa la MO? Kasajiliwa Akpan ka-flop ni faida ama hasara? Walikuwepo wakina Okrah wakafeli, wahesabu na Wachezaji wazawa waliofeli na kuondoka! Hujataja Makocha na Waajiri! Kuna faida hapo? Ni vile tu hatukubali ukweli mchungu.

Timu haisajili Wanachama maana yake 49% zake tu ndizo zinafanya kazi, Mashabiki wao ni kununua jezi na uwanjani pekee, unatarajia asiingize hasara hapo? Kwanini tuchukie anaposema ni mali yake?Hata kwenye diin Mwanamke usiyemhudumia sio wako.

Mpira duniani bado ni UFUKARA! Gharama ya kuifanya Simba kuwa timu kubwa ni lazima inampa hasara kubwa mno MO, kama ambavyo Roman Abramovich alivyopambana kuijenga Chelsea ilimbidi mpaka akafungue akaunti huko Virginia ili timu ipokee pesa ya zaidi na ameondoka ANAIDAI Chelsea.

 

 

Leave A Reply