The House of Favourite Newspapers

Ni Mnyama Gani Aliyesambaza Virusi vya Corona?

0

TAFITI za Kisayansi zimethibitisha kuwa kuna mnyama ambaye alimbaza virusi vya corona kutoka kwa popo hadi kwa binadamu. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema utafiti huo umelenga chimbuko la virusi hivyo, baadhi ya wanasayansi wanasema huenda isifahamike namna ambavyo mtu wa kwanza aliambukizwa virusi hivyo.

 

Bado haijafahamika ikiwa mnyama aliyesambaza virusi hivyo aliuzwa katika soko la wanyama pori la Wuhan nchini China ambalo kwa sasa limejitia dosari.

 

Watafiti wanasema biashara ya wanyama pori inatoa fursa ya usambaaji wa magonjwa kutoka kwa spishi moja hadi nyengine ambako kulisababisha milipuko kadhaa iliyopita na imelaumiwa kwa janga hili la corona.

 

Afisa wa Shirika la Afya Duniani anayehusika na utafiti wa Covid-19, Dkt. Maria Van Kerkhove, ameiambia BBC katika kipindi cha Andrew Marr show: “Tunajitayarisha kukabiliana na janga kama hili kwasababu sio suala la ikiwa linaweza kutokea, badala yake ni lini litatokea.”

 

Maambukizi ya Virusi

Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza wanakubali kwamba kama magonjwa mengine yanayojitokeza, virusi hivi awali vilisambaa bila kugundulika kati spishi moja hadi nyengine. Profesa Andrew Cunningham, kutoka Chama cha Hifadhi ya Wanyama cha Uingereza, anaelezea: “Kwa muda mrefu tumekuwa tukitarajia kuwa kitu kama hiki kinaweza kutokea.

“Magonjwa kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika miaka ya hivi majuzi kwasababu ya wanadamu kuvamia makao ya wanyama hao na kuongezeka kwa utangamano na watu kutumia wanyama pori.”

 

Virusi vinavyosababisa Covid-19 havijakaribiana na mlipuko wa kwanza wa virusi kama hivyo. Inaingia kwenye orodha ya vinavyosababisha magonjwa kama vile Ebola, kichaa cha mbwa, Sars na Mers – ambayo chanzo chake ni popo wa mwituni.

 

Baadhi ya ambayo kwasasa hivi ni ushahidi kuhusu virusi vya popo na uwezo wa kuambukiza mwanadamu kunatokana na utafiti wa mlipuko wa ugonjwa wa Sars uliotokea 2003 wenye uhusiano wa karibu na virusi vya corona.

 

Kinachohitajika kwa virusi ili viweze kuambukiza mtu mwengine mpya ni uwezo wa chembe kuingia ndani na kuanza kuzaliana. Na kama ilivyo kwa ugonjwa wa Sars, popo mwenye kusemekana kuwa chanzo cha virusi vya corona alikuwa na uwezo wa kuingia kwenye seli za binadamu.

 

“Kwa ugonjwa wa Sars-CoV-2 cha msingi ni protini ya virusi inayoitwa Spike na ili kuweza kuingia kwenye seli au chembe unahitaji kipokezi mfano wa funguo katika usemi wa kawaida. Kipokezi hicho kinajulikana kama ACE2,” ameelezea Profeesa David Robertson, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka chuo kikuu cha Glasgow.

 

“Virusi vya corona sio kwamba vinaweza kuingiliana vizuri na kipokezi cha ACE2, “Hali hii imekuwa ikitokea mara nyingi hata kuliko virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Sars-1”, amesema.

 

Na kwasababu hiyo, ni wazi kwamba virusi vya corona ni rahisi sana kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine; ni ugonjwa wa kuambukiza ambao umekuwa changamoto kudhibitika. Lakini hadi kuleta karibu virusi vya popo kwa seli ya mwanadamu hapo ndipo biashara ya wanyama pori inaposemekana ilichangia kwa kiasi kikubwa sana.

 

Kununua, kuuza na kuambukiza

Wengi wetu tumesikia kwamba virusi hivyo vilianza katika soko la wanyama pori mjini Wuhan. Lakini chanzo cha virusi hivyo – mnyama mwenye viini hivi mwilini mwake hakupatikana sokoni.

 

“Maambukizi ya awali yalihusishwa na soko – ushahidi wa uhakika,” anaelezea Profesa James Wood kutoka chuo kikuu cha Cambridge.

 

“Huenda maambukizi yalitokea kwengineko na kwa bahati mbaya yakafika sehemu iliyokuwa na wanadamu. Lakini kwasababu ni virusi vinavyotoka kwa wanyama, kwa kiasi kikubwa chanzo huenda kikawa soko hilo.”

 

Profesa Cunningham anakubali kwamba; Masoko ya wanyama, ni kitovu cha magonjwa ya wanyama kuambukiza wengine.

 

 

“Kuchanganya idadi kubwa ya spishi katika mazingira machafu na spishi na wanyama ambao kwa hali ya kawaida huwa hawachanganyikani hilo linachangia viini kutoka kwa spishi moja hadi nyengine,” anaelezea.

 

Siku za nyuma, virusi vingi vilitoka kwa wanyama pori hadi kwa binadamu kupitia spishi nyengine – ambayo ama inafugwa au inawindwa na kuuzwa sokoni.

 

Profesa Woods anaelezea: “Chimbuko halisi la virusi vya Sars hadi kwa mwanadamu kulitokana na mlipuko ambao chanzo chake kilikuwa ni mnyama fungo ambao walikuwa wanauzwa kusini mwa China kama mlo.

 

 

“Hilo lilikuwa muhimu kulifahamu kwasababu kulikuwa na mlipuko wa hao fungo wenyewe na kulazimisha hatua za kudhibiti biashara hiyo kuchukuliwa ili kusitisha kile ambacho kilikuwa ni uwezekano wa virusi kusambaa hadi kwa mwanadamu.”

 

Kuendelea kutafuta kile kisichojulikana kuhusu vile ugonjwa huu wa Covid-19 ulivyofika kwa binadamu, wanasayansi walichukulia wanyama hawa minki, chororo kaya na kasa kama kidokezo kinachoweza kufikia ukweli wa chimbuko la Covid-19.

 

Virusi kama hivyo vilipatikana katika miili ya mnyama kakakuona ambao ni nadra sana lakini kati ya hao ambao wanashukiwa hakuna aliyeonesha kwamba amehusika na mlipuko wa virusi vya corona.

 

 

Tunachofahamu ni kwamba kutangamana kwetu na wanyama pori kunatuweka sisi na wao katika hatari.

“Kuhakikisha kwamba wanyama pori hawatangamani moja kwa moja na mwanadamu au na wanyama wengine wa nyumbani ni jambo la msingi,” amesema Profesa Wood.

 

Ingawa kuthibiti biashara ya wanyama pori kote duniani sio jambo linaloweza kutekelezeka moja kwa moja.”

 

“Kumekuwa na kampeni kadhaa ya kupiga marufuku biashara zote za wanyama pori na kutangamana nao,” amesema Profesa Wood.

 

“Lakini sasa kile kitakachotokea ni kuadhibu baadhi ya watu maskini zaidi duniani.

Mara nyingi, kuchukua hatua kama hizo kitakachotokea ni biashara hiyo kufanyika kisirikisiri na kufanya iwe vigumu zaidi kufanya lolote katika kukabiliana na hali hiyo.”

 

Shirika la Afya Duniani tayari limetoa wito wa kutekelezwa kwa usafi wa hali ya juu na kuimarishwa kwa usalama katika masoko ya bidhaa za vyakula vya kuharibika haraka nchini China. Lakini mara nyingi – biashara kama ile ya wanyama pori katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako kulihusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola – masoko hayako rasmi na hivyobasi, ni vigumu kutadhibiti.

 

“Hilo haliwezi kufanyika ukiwa ofisini Uingereza au mjini Geneva; linafanyika tu katika eneo kwa kila nchi,” Profesa Wood aliongeza.

 

Dkt. Maria Van Kerkhove alikubali kwamba “Ni muhimu sana kushirikiana na watu ambao kazi zao zinashirikisha uuzaji wa wanyama kwa binadamu – watu wanaofanyakazi inayohusisha wanyama pori.”

 

Kinachotokea na juhudi za kimataifa zenye pingamizi chungu nzima. Lakini, mlipuko wa Covid-19 umedhihirisha gharama ya mbadala.

Leave A Reply