The House of Favourite Newspapers

Ni Sahihi Wazazi Kukuchagulia Mke/Mume? Soma Hapa

NIANZE kwa kumshukuru Mungu kwa kuniweka hali mpaka siku hii nzuri ya leo. Ni matumaini yangu kwamba na wewe msomaji wangu, u mzi­ma buheri wa afya na unaende­lea vyema na majukumu yako ya kila siku. Wewe ambaye afya inaleta matatizo, nakuombea upone haraka.

Je, upo kwenye uhusiano wa kimapenzi, unampenda sana mume, mke, mchumba au mpen­zi uliyenaye lakini wazazi wako hawamkubali na matokeo yake wanakuchagulia mtu wa kuishi naye?

Mada ya leo ni kwa ajili ya wewe msomaji wangu ambaye upo kwenye mazingira kama haya, ya wazazi kumkataa umpendaye kwa sababu ambazo wanazijua wao. Kwa ambao wamewahi kupi­tia changamoto hii au bado wapo ndani yake, watakuwa wanaelewa vizuri ugumu uliopo linapokuja suala kama hili.

Wazazi wako wamekuzaa na kukulea tangu ukiwa mdogo mpa­ka umekuwa mkubwa, umempata umpendaye lakini wao wanam­kataa na kukwambia unatakiwa kuchagua moja, wao (wazazi) au huyo unayempenda. Utachukua uamuzi gani? Utamuacha kwa sababu wazazi hawampendi? Utakubali kuwadharau wazazi wako na kuendelea naye?

Bila shaka kila mmoja atakuwa na jibu lake tofauti, lakini tuna­chokihitaji hapa, ni kujadiliana, kupanuana mawazo, kupeana uzoefu ili mwisho kila mmoja awe na uwezo wa kuivuka changa­moto hii kwa sababu hata kama bado haijakukuta, huenda ipo siku na wewe yatakutokea.

Hebu soma ushuhuda wa mso­maji wangu mmoja ambaye yupo kwenye hali mbaya na anahitaji ushauri:

“Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 42, nilioa miaka kumi iliyopita na tumejaliwa kupata watoto wawili. Tatizo li­nalonisumbua na kuniweka njia panda, wazazi wangu hawamku­bali kabisa mke wangu badala yake kuna mwanamke mwingine ambaye ndiyo wao wanataka mimi nimuoe. Naomba ushauri, nifanyeje?”

Amehitimisha msomaji wangu huyu, bila shaka umemuelewa. Najua huyu ni mmoja tu la­kini wapo wengi ambao wa­natokewa na visa kama hivi. Naomba tujadiliane pamoja, ungekuwa ni wewe kwenye na­fasi ya msomaji huyu, ungefan­ya nini? Kama ungepewa kazi ya kumshauri, ungemwambia nini?

Hakuna chuki ambayo huwa haina chanzo. Kama mumeo, mkeo anachukiwa na wazazi wako, jambo la kwanza ambalo unatakiwa kulijua, ni kwamba lazima kuna chanzo kilicho­sababisha hali hiyo. Na kama yalivyo matatizo mengine yote, huwezi kupata muafaka kama hujakijua chanzo.

Wengi hushindwa kutumia busara katika kutafuta chan­zo. Yawezekana umpendaye ndiyo chanzo cha kuwafanya wazazi wako wasimkubali ila kwa sababu ya mapenzi yako kwake, unaukataa ukweli na kumtetea. Hutaweza kupata suluhu, matokeo yake utajiku­ta unawachukia wazazi wako mwenyewe.

Yawezekana pia wazazi wako ndiyo tatizo lakini kwa sababu ya malezi uliyopewa, huwezi kum­kosoa mzazi wako. Mwingine atasema anaogopa laana ya wazazi kwa hiyo hata kama anajua tatizo linaanzia wapi, hatakuwa na uthubutu wa kulizungumza, matokeo yake, ataungana na wazazi wake mwisho ataach­ana na ampen­daye na kwenda kuoa mwanamke asiyempenda.

Tukutane wiki ijayo kuangalia se­hemu ya pili ya mada hii kujua nini una­p a s w a k u f a n y a u n a p o k u ­tana na changa­moto kama hii. Kama una mao­ni, ushauri au swali, nicheki kwa namba za hapo juu.

Comments are closed.