The House of Favourite Newspapers

Niger: Utawala wa kijeshi unatishia kumuua Bazoum iwapo ECOWAS itaingilia kijeshi

0
Rais wa Niger aliyeondolewa mamlakani na jeshi Mohamed Bazoum.

Mvutano unazidi kuongezeka kati ya utawala mpya wa kijeshi wa Niger na jumuiya ya ukanda wa Afrika Magharibi ambayo imeamuru kutumwa kwa wanajeshi kurejesha demokrasia nchini humo.

Jumuiya ya ECOWAS ilisema Alhamisi kuwa umeamua kupeleka “kikosi cha kukaa tayari” kinacholenga kurejesha utaratibu wa kikatiba nchini Niger, baada ya muda wa masharti yake ya kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum kumalizika Jumapili.

Mapema Jumamosi, maafisa wawili wa nchi za Magharibi waliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba utawala wa Niger ulimwambia mwanadiplomasia mkuu wa Marekani kwamba wangemuua Bazoum ikiwa nchi jirani zitajaribu kuingilia kati kijeshi kurejesha utawala wake.

Haijulikani ni lini au wapi kikosi cha ECOWAS kingetumwa, na jinsi ripoti za vitisho dhidi ya Bazoum zingeathiri uamuzi wa jumuiya hiyo yenye wanachama 15 kuingilia kati. Wataalamu wa mizozo wanasema kikosi hicho kinaweza kuwa na wanajeshi 5,000 wakiongozwa na Nigeria, na kinaweza kuwa tayari ndani ya wiki chache.

Baada ya mkutano wa ECOWAS, rais wa nchi jirani ya Ivory Coast, Alassane Ouattara, alisema nchi yake itashiriki katika operesheni hiyo ya kijeshi, pamoja na Nigeria na Benin.

Leave A Reply