The House of Favourite Newspapers

Ninja: Bado Nina Mavitu Mengi

Shaibu Ramadhani ‘Ninja’.

BEKI wa kati wa Yanga anayekuja kwa kasi, Shaibu Ramadhani ‘Ninja’ amesema bado ana vitu vingi vya kuifanyia klabu yake hivyo mashabiki watulie wasubiri vitu hivyo kutoka kwake.

 

Ninja ametoa kauli hiyo baada ya kuanza kuaminika katika kikosi hicho kinachonolewa na Kaimu Kocha Noel Mwandila na kupata nafasi kikosi cha kwanza.

 

Beki huyo, katika michezo miwili iliyopita ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia alionza kikosi cha kwanza na kufanya vizuri.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ninja alisema ili afanikishe hayo aliyoyaahidi ni lazima viongozi na mashabiki wamuamini anapokuwa uwanjani ili ajenge hali ya kujiamini na kupambana.

 

Ninja alisema, amepanga kuleta mabadiliko makubwa ndani ya timu hiyo na hilo linawezekana kwake kutokana na kujipangia muda wa mazoezi ya ziada.

 

“Nawashukuru makocha wangu kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kucheza kikosini, kwani hayo yalikuwa ndiyo malengo yangu ya kucheza kikosi cha kwanza.

 

“Nina kazi kubwa ya kuendelea kupambana katika timu kwa kuhakikisha ninatimiza majukumu yangu ya uwanjani ili nisiondolewe kikosi cha kwanza.

 

“Bado nina vitu vingi vya kuwaonyesha mashabiki wa Yanga na licha ya ushindani uliopo kila ninapopata nafasi kikosini nitajitahisi kuvionyesha kwani ndiyo malengo yangu,” alisema Ninja anayecheza Yanga msimu wa kwanza akitokea Jang’ombe Boys ya Zanzibar.

Comments are closed.