The House of Favourite Newspapers

NISHA AMFANYIA KITU MWANAYE CHINA

Salma Jabu ‘Nisha’

LICHA ya watu wengi kulalamika maisha magumu, msanii wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ hivi karibuni aliamua kufanya kufuru kwa mwanaye, Ipsium (14) katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ nchini China.

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Nisha alisema kwenda kumfanyia mwanaye sherehe China ni kwa sababu

ndiye kila kitu kwake kwani anaye huyo pekee hivyo anamfanyia kile kitu kinachomfurahisha maishani mwake ili afurahie uwepo wake.

 

“Mwanangu nimemfanyia sherehe ya bethidei China ambayo imegharimu milioni nane, tumekuja kufanya huku maana ndipo alipopachagua nami kwa kuwa nampenda na ndiye mwanangu wa pekee nikamleta na amefurahi sana na anajivunia kuwa na mama kama mimi pia nafurahi kuwa na mtoto mkubwa hivi kwa sasa,” alisema Nisha.

LAVALAVA: “Diamond Ana Mapungufu / Tunavumilia / Alikiba…”

Comments are closed.