The House of Favourite Newspapers

Niyonzima Avutiwa Na Rutanga Yanga

0
Haruna Niyonzima.

KIUNGO mchezeshaji fundi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa ujio wa beki wa kushoto wa Polisi Rwanda ya nchini humo, Eric Rutanga, utaimarisha kikosi chao kwenye safu ya ulinzi.

 

Rutanga anayeunda kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, ni mchezaji wa kwanza wa kimataifa kuanza kusajiliwa na Yanga katika kuelekea msimu ujao akisaini kwa dau la dola 25,000 (karibu Sh milioni 60).Beki huyo mwenye uwezo wa kuanzisha mashambulizi, kukaba na kupiga krosi zenye macho kwa wachezaji wenzake, atatua Yanga huku akiwa na uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza baada ya timu hiyo kumkosa mchezaji wa aina yake.

 

Eric Rutanga

Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema kuwa mabosi wake hawajafanya makosa kumsajili Rutanga, hiyo ni kutokana na kiwango kikubwa alichonacho beki huyo ambaye aliwahi kucheza naye timu ya taifa ya Rwanda.

Niyonzima alisema kuwa timu yao ilimkosa beki wa kushoto mwenye uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi, pia upigaji wa krosi nzuri kama alivyo nahodha msaidizi wa timu hiyo, Juma Abdul anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga krosi.

 

Aliongeza kuwa timu hiyo ilimkosa beki wa aina hiyo ya Rutanga, hivyo ujio wake utaimarisha kikosi chao katika kuelekea msimu ujao ambao wamepanga kuchukua ubingwa wa ligi.

 

“Ninaufahamu vizuri uwezo wa Rutanga, ni kati ya mabeki bora wa pembeni namba tatu Rwanda, nimesikia taarifa zake za kuja kuichezea Yanga msimu ujao.

 

“Ujio wake utaimarisha kikosi chetu kwani sina hofu juu ya uwezo wake wa ndani ya uwanja, hivyo ninaamini akijiunga na Yanga, tutakuwa na safu nzuri ya ulinzi.“Rutanga ana uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi na kupiga krosi kwenye goli la wapinzani, ninamfananisha na Abdul kwenye uwezo wa kucheza nafasi ya beki ya pembeni, hivyo mashabiki wamsapoti mara atakapojiunga na timu,” alisema Niyonzima.

STORI: WILBERT MIOLANDI, Dar es Salaam

TIMU YA SIMBA YAAPA KUPATA UBINGWA JIJINI MBEYA BAADA YA KUCHUKUA POINTI 6

Leave A Reply