The House of Favourite Newspapers

Niyonzima, Mbonde Waanza Mazoezi Rasmi

KIUNGO machachali wa Simba, Haruna Niyonzima ambaye alikuwa ameingia kwenye hofu ya kukosa msimu kucheza mzima amejiunga na wachezaji wenzake na kuanza mazoezi ya uwanjani.
Niyonzima alisafiri hadi India ambako alipatiwa matibabu ambaye yameondoa hofu ya kuukosa msimu hadi mwisho na sasa ameanza mazoezi ya uwanjani lakini kwa kuzunguka pembeni ya uwanja.
Mbali na Niyonzima, beki Salim Mbonde wa Simba aliyekuwa amepata majeraha kwa ajali ya pikipiki naye ameanza mazoezi na wenzake. Hata hivyo, Mbonde amekuwa akizunguka uwanja pembeni kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya kuungana na wenzake.
Niyonzima na Mbonde walikuwa wakizunguka uwanja wakati Simba ikijifua leo jioni kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

PIGO SIMBA: MKUDE Alivyotoka Machozi Mazoezini Baada ya Kuumizwa

Comments are closed.