The House of Favourite Newspapers

Njemba lataka kubadili jina la Taylor Swift kisa la kike

980xTaylor Swift.

JAMAA mmoja anayojulikana kama Taylor Swift ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kutaka kubadili jina hilo kisa linatumiwa na staa wa Pop, Taylor Swift ambaye ni mwanamke.

Jamaa huyo mwenye miaka 30, anatokea Washington, Marekani na katika mahojiano aliyofanyiwa hivi karibuni na kituo kikubwa cha habari cha NBC alisikika akisema kuwa amekuwa katika wakati mgumu kufanananishwa jina hilo na la mwanamuziki.

“Nimeshaingia katika mtandao wa google na kutafuta kurasa kama 10,000 zote zinamtambua Swift (Taylor) yule wa kike ambaye ni mwanamuziki na hata nikiangalia kwenye mitandao mingi iko hivyo,” alisema jamaa huyo.

Katika utafiti uliofanywa na kituo hicho cha NBC watu zaidi ya 60 wanaotumia jina la Taylor Swift wana miaka kati ya 20 hadi 60 kwa hivyo kitendo cha Taylor mwanaume kuendelea kutumia jina hilo kinamkosesha barua pepe nyingi ambazo moja kwa moja zinakwenda kwa Taylor msanii.

(Imetayarishwa na Andrew Carlos/GPL)

Comments are closed.