NMB Yaipa Serikali Sh 750 Milioni Mkutamo Mkuu wa ALAT

Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – filbert Mponzi (Kushoto) akikabidhi mfano wa Hundi kwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa – Mh Gulamhafeez Mukadam ikiwa ni ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa unaotegemewa kuanza leo jijini Mwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – John Magufuli. Wa pili kushoto ni Mkuu wa KItengo cha Huduma za Serikali – NMB – Vicky Bishubo na Katibu Mkuu wa ALAT – Elirehema Kaaya. NMB ndiye Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa.

BENKI ya NMB imesaidia zaidi ya Sh 750 milioni kwaajili ya Mikutano Mikuu ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (ALAT) kwa miaka mitano mfululizo huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na serikali za mitaa nchini kutatua changamotoi mbalimbali.

 

Akizungu jana jijini Mwanza katika zoezi kukabidhi fedha hizo, Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Filbert Mponzi alisema kuwa  wamefika uamuzi huo kutoakana na benki hiyo kutambua mausiano mazuri ya kibiashara yalipo kati yao na Alat.

 

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ALAT unataeajiwa kuanza kesho Jumatatu katika Hoteli ya Malaika Beach jijini Mwanza.

 

Mponzi alisema kuwa benki hiyo inatambua mahusiano ya kibiashara yaliyopo kati ya NMB na ALAT kupitia zaidi ya halmashauri 180 ambapo benki inashiriana kukusanya mapato ya serikali huku akisema kusema kuwa taasisi hiyo ni mmbia wa karibu na serikali, hivyo mahusiano ya NMB na ALAT yameanza muda mrefu uliopita.

 

“TunaishukurusekretarietyaAlatpamojanawajumbewotekwakuendeleakutoaushirikiano, kufanyabiasharapamojanasisikamabenkitumekuwatukiendeleakuboreshahudumazetuilikuwezakuhudumiaserikalikuupamojanaserikalizamitaa,” alisemaMponzi

 

“Tumepeleka huduma zetu nchi nzima huku tukizifikia Zaidi ya halmashauri 180 tukiwahudumia katika Nyanja mbalimbali za kibenki kuanzia wafanyakazi, wafanyabiashara na wajasiliamari  na pia madiwani nah ii inaonyesha utayari wetu wa kuhudumia Serikali za mitaa.”

 

Mwenyekiti wa ALAT taifa – Gulamhafeez Mukadam ameishukuru Benki ya NMB kwa kuonyesha kujali serikali za mitaa na mchango wa mwaka huu unaonyesha dhamira na ushirikiano wa kweli kati ya taasisi mbili.

 

Mukadam aliongeza kuwa jamii za Serikali za mitaa na mamlaka zake bado zinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kushikwa mkono na taasisi kama NMB kwaajili ya kusaidiana kutatua changamoto hizo.

 

“Nafikiria benki inaweza sasa ikabadiri muelekeo wake kuhusu misaada mbalimbali kwa jamii, kwa kuhakikisha wanachukua mradi hata mmoja mkubwa kwenye wilaya na kuhakikisha wanaukamilisha kwa usimamizi wao ambao utaleta ile thamani halisi ya fedha wanazotoa.” Alisema Mukadam.

UTASHANGAA!!! BABU wa MIAKA 100, HAJAOA, Hana MTOTO..


Loading...

Toa comment