The House of Favourite Newspapers

NMB Yashinda Kwenye Mkutano wa 25 wa Wanachama wa PPF

0

PPF 3

Picha ya pamoja ya washindi mbalimbali waliojinyakulia tuzo katika Mkutano Mkuu wa 25 wa Mfuko wa PPF uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. NMB iliibuka mshindi wa jumla kati ya taasisi zilizoshindanishwa katika tuzo ya uchangiaji bora wa michango ya wafanyakazi kwenye mfuko wa PPF nchini kwa mwaka 2015.

PPF 2Naibu waziri wa Fedha na Mipango – Ashatu Kijaji akikabidhi tuzo ya ushindi wa jumla kwa Afisa Mkuu wa rasilimali watu wa NMB (Chief Human Resource Officer) – Charles Kazuka wakati wa mkutano mkuu wa 25 wa mfuko wa PPF. Katika mkutano huo, NMB iliibuka mshindi wa jumla kati ya taasisi zilizoshindanishwa katika tuzo za uchangiaji bora wa michango ya wafanyakazi kwa mfuko wa PPF nchini kwa mwaka 2015. Mbali na ushindi wa jumla, pia NMB ilishinda tuzo ya mchangiaji mkubwa na mwajiri mwenye idadi kubwa ya wafanyakazi kwenye mfuko huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF – William Urio na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii za bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – Richard Ndasa wakishuhudia katika hafla iliyofanyika jana jijini Dar es salaam.

PPF 1 (1)Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakionyesha tuzo ambazo Benki hiyo imejinyakulia katika Mkutano Mkuu wa 25 wa Mfuko wa PPF leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni mkuu wa kitengo cha rasilimali za watu, Afisa Mkuu wa rasilimali watu wa NMB (Chief Human Resource Officer) – Charles Kazuka na Meneja Muandamizi wa huduma za rasilimali watu Emmanuel Akonaay

PPF 4

Meneja Muandamizi wa huduma za rasilimali watu Emmanuel Akonaay akipokea tuzo kutoka kwa Naibu waziri wa Fedha na Mipango – Ashatu Kijaji.

 

Benki ya NMB imeshinda tuzo tatu katika Mkutano wa 25 wa Mwaka wa wanachama wa PPF iliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NMB imetajwa kuwa mshindi wa jumla katika ulipaji mapema ya michango ya wanachama kwa mwaka 2015. Benki pia iliibuka nafasi ya kwanza na kutambuliwa kuwa ni Mwajiri mwenye mchango mkubwa katika mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili katika kundi la Mwajiri mwenye idadi kubwa ya wanachama hai wanaochangia mfuko wa PPF.

Ushindi huo unadhihirisha ukweli kwamba NMB ndiyo beki kubwa kuliko zote nchini yenye matawi zaidi ya 170 na ATM zaidi ya 600 nchini kote huku ikijivunia hazina ya wateja zaidi ya milioni mbili nchini kote. NMB ina wafanyakazi zaidi ya 3000 ambao ndio wameipa ushindi benki katika tuzo zenye heshima hapa nchini zinazotolewa na mfuko wa pensheni wa PPF.

Leave A Reply