The House of Favourite Newspapers

NMB Yawaandalia Hafla Fupi Wabunge, Yawapongeza Kwa Kuchaguliwa Kwao

0
Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson akikaribishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dk. Edwin Mhede.

Benki ya NMB jana imeandaa hafla maalum jijini Dodoma ya kuwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la 12, lililozinduliwa hivi karibu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kuwapongeza kwa kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi na kuwatakia safari njema katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati) akimkaribisha Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Benard Kibesse.
Wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dk. Edwin Mhede(kulia), Afisa Mkuu wa Wateja
Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi(kushoto) na Mkuu wa Idara wa Mawasiliano wa NMB, Eunice Chiume.

 

Hafla hiyo, ilizinduliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Tulia Ackson aliyekuwa Mgeni rasmi. Benki ya NMB ilitumia fursa hiyo kuwajulisha Waheshimiwa Wabunge namna wanaweza kufaidika na huduma nyingi za NMB ikwemo; mikopo maalum, uwekezaji, bima mbalimbali, na matumizi mbadala ya kibenki kama NMB Mkononi.

c

Baadhi ya wabunge wakiwa katika hafla hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema, moja ya malengo ya Benki hiyo ni kuhakikisha wanashirikiana na wadau katika kujenga taifa bora lenye uchumi imara kupitia sekta ya kibenki. Dhamira ya NMB ni kuendelea kushiriki katika miradi ya maendeleo katika majimbo yao na taifa kwa
ujumla.

Vile vile, Dk. Tulia aliipoongeza Benki hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma zake na kujitanua kiutendaji katika kila eneo hapa nchini huku akitambua mchango wa NMB katika jamii.

 

Wakiwa Dodoma, Zaipuna na Mponzi walishuhudia uzinduzi wa Bunge la 12, na vile vile kupata nafasi ya kumtembelea Kamishna Generali wa Magereza nchini, Suleimani Mzee katika ofisi yake.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati) akiwa ofisini kwa Kamishna Generali wa Magereza nchini, Suleimani Mzee. Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi.

 

Leave A Reply