The House of Favourite Newspapers

Nmb Yazindua Huduma za Kibenki Kwa Wana Diaspora

0

  • Jisikie upo nyumbani popote utakapoenda duniani na ‘NMB Kwetu’

Tumezindua rasmi dirisha la huduma za kibenki kwa watanzania waishio nchi za nje yaani Wana Diaspora inayojulikana kama NMB Kwetu.

Kuhakikisha urahisi, tumetengeneza mfumo wa kidijitali wa ukusanyaji wa nyaraka utakaowawezesha Wana Diaspora kujaza taarifa zote zinazohitajika kwa njia ya mtandao ili kufungua akaunti – openaccount.nmbbank.co.tz

Kupitia huduma mahsusi za NMB Kwetu, wanadiaspora watanufaika na:

  • Bima ya maisha yenye thamani ya hadi Shilingi za Kitanzania Milioni 29, bila gharama za ziada – kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance.
  • Hakutakuwa na makato ya mwezi (monthly fees) kwa akaunti za diaspora.
  • World Wide Pesa – Tuma pesa nyumbani kwa ndugu, jamaa na marafiki kutoka nchi zaidi ya 100 duniani – kwa kushirikiana na Makampuni mahiri ya Thunes na Terrapay.
  • Fursa ya kupata mikopo ya nyumba (kununua ama kujenga nyumba).
  • Fursa za kuwekeza kwenye amana za muda mfupi na amana za muda mrefu zenye viwango shindani.
  • Kutumia huduma za kidijitali za Benki ya NMB kufanya miamala popote walipo duniani.

Uzinduzi huu umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki – Balozi Stephen Mbundi na Afisa Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna.

Leave A Reply