The House of Favourite Newspapers

NMB Yazipiga Jeki Wilaya Za Mufindi, Rorya, Kilolo na Arusha

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kihaka wilayani Kilolo – Iringa wakiwa wamebeba stuli za maabara muda mfupi baada ya kukabidhiwa na benki ya NMB. Benki ya NMB ilikabidhi meza na stuli 60 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Chacha  akiwa ameketi na wanafunzi  wa shule ya Msingi Minigo juzi (Jumanne) katika moja ya madawati yaliyotolewa na benki ya NMB  ili kusadia kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo. Wengine ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa (Mwenye koti na Tai Nyeusi), Amos Mubusi.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Maduma iliyoko Kata ya Maduma Wilayani Mufindi wakishangilia madawati waliyokabidhiwa na benki ya NMB juzi shuleni kwao.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mrisho Gambo ya jijini Arusha wakati wa hafla ya kukabidhiwa meza na viti vyenye thamani ya shilingi 10 milioni vilivyotolewa na benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro.

 

Comments are closed.