The House of Favourite Newspapers

NSSF Yazindua Kampeni ya ‘Boresha Taarifa’ kwa Wanachama – Video

Meneja Meneja Kiongozi Mahusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele na Meneja Matekelezo na Uanachama wa NSSF, Joseph Fungo, wakizungumza na +255 Global Radio. 

 

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) liko katika mchakato wa kuboresha taarifa za wanachama wake.

 

….Wakizungumza na wafanyakazi wa Makampuni ya Global Group.

Hayo yamsemwa leo na Meneja Meneja Kiongozi Mahusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele wakati akizungumza na kituo cha radio cha 255 Global Radio wakati alipotembelea ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori jijini Dar s Salaam ili kujionea zinavyofanya kazi na kufikisha ujumbe wake huo.

 

Meneja Meneja Kiongozi Mahusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele wakati akizungumza na kituo cha radio cha 255 Global Radio wakati alipotembelea ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori

Mengele na Fungo wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa Global Radio, Lucas Masungwa (kushoto), Dar Boy (katikati) na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Janet Ezekiel.

 

“Zoezi hili litahitaji kuunganisha taarifa za wanachama zilizo katika Mfuko na taarifa zilizopo katika kitambulisho cha Taifa. Katika zoezi hili Shirika limekuja na kampeni ya Boresha Taarifa na NSSF,” alisema Mengele.

 

Aliongeza kwamba katika zoezi hili mwanachama atatakiwa kutumia namba yake ya kitambulisho cha Taifa kwa mwajiri wake, au kuwasilisha mwenyewe namba ya kitambulisho cha Taifa katika ofisi za NSSF zilizo karibu naye ili kuweza kuboresha taarifa zake NSSF.

 

 

“Tunataka wanachama wetu waboreshe taarifa zao kwa kuoanisha taarifa ambazo tunazo katika shirika la NSSF na pia ambazo zipo katika kitambulisho cha Taifa.

 

 

Akifafanua zaidi alisema baada ya madadiliko ya sheria katika sekta ya hifadhi ya jamii iliyofanyika mwaka 2018, NSSF inawaandikisha wananchi wote kutoka sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi na hivyo katika sekta binafsi wafanyakazi wote wanaokuwa wameajiriwa kwa muda mfupi au mrefu waajiri wao wanatakiwa kuwaandikisha NSSF.

 

Lakini pia, alisema,  NSSF imepewa jukumu la kuandikisha wananchi wote waliojiajiri wenyewe na kwamba kampeni ya sasa ni kwa ajili ya wafanyakazi wote wa serikali, makampuni binafsi, na wafanyabiashara wadogo.

Wakiserebuka ndani ya Studio za +255 Global Radio.

 

Naye Meneja Matekelezo na Uanachama, Joseph Fungo, alisema kwamba: “Moja ya vitu vikubwa vinavyochelewesha mafao ni taarifa na ndiyo maana tukasema ili tufikie kumlipa mwanachama huyu kwa wakati,  basi kwanza turekebishe taarifa zake akiwa kazini kwani changamoto inakuja unapokuwa umeshatoka kazini na taarifa haziko sawa hivyo, mambo yanakuwa magumu sana.”

 

Meneja Matekelezo na Uanachama wa NSSF, Joseph Fungo, akizungumza na kituo cha radio cha 255 Global Radio.

 

Alisisitiza kwamba huu ni wakati sahihi wa wahusika kwenda kurekebisha taarifa ili siku wanapokuwa wametoka kazini mafao yao yaeleweke kwa haraka.

 

Wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) na Mkuu wa Vipindi Global Radio, Borry Mbaraka.

 

Wakizungumza na wafanyakazi wa Global Group.

 

Mengele ndani ya Studio za Global Radio.

 

Fungo akisaini katika kitabu cha wageni.

 

 

Mengele akisaini katika kitabu cha wageni.

Comments are closed.