The House of Favourite Newspapers

NUH MZIWANDA APOTEZWA NA LAANA

‘Nuh Mziwanda’

MWANAMUZIKI Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye mbali na kazi nzuri anazofanya aliingia kwenye masikio, macho na midomo ya watu baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanadada Zuwena Mohamed ‘Shilole.’ Hata hivyo, penzi lao baadaye liliota mbawa na kupaa, wakamwagana.

Kila mmoja akachukua hamsini zake na Nuh akazama kwenye penzi lingine la mwanadada aitwaye Nawal ambaye baadaye walipata mtoto mmoja wa kike. Lakini pia uhusiano wa wawili hao baadaye ulitawaliwa na changamoto zilizosababisha kila mmoja ajikate kivyake, wakabaki wanalea mtoto. Maisha yakasonga mbele na hivi karibuni Nuh amerudi tena kuvuma!

Unajua ni kwa nini? Kama hujui ni kwamba ulisambaa ujumbe kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, unaonyesha kwamba mzazi mwenzake huyo alikuwa anazungumzia kumlaani kutokana na kutokumsikiliza, jambo ambalo linadaiwa eti linasababisha mpaka muziki wake usifike mbali kwa sasa. Watu wengi walitoa maoni yao katika ujumbe huo, Showbiz Xtra, pia iliona isiwe kesi, ikaamua kumsaka Nuh ili aweze kuzungumzia suala hilo pamoja na mambo mengine kuhusu muziki wake na maisha kwa ujumla. Huyu hapa:

Showbiz: Umepunguza makeke na huvumi kwenye media kama zamani, nini tatizo?

Nuh: Hakuna tatizo. Niliamua kukaa kimya bila kuachia kazi, pia niliamua kukaa mbali na skendo ndiyo maana inaonekana sina makeke tena.

Showbiz: Ni kweli unapotezwa kimuziki na Nawal? Maana anadai amekupa laana.

Nuh: (Ana-cheka) Dah! Kivipi tena, kwa kipi nilich-okifanya kwake hadi anipe laana. Kwanza yeye siyo ma-ma yan-gu mzazi wala Mungu, hivyo hawezi kunipa laana.

Sh-ow-biz: Lakini umeona ujumbe uliosambaa Instagram juu ya Nawal kukulaani na maoni ya watu waliyotoa?

Nuh: Nimeona, lakini akaunti iliyoandika ujumbe ule si ya Nawal, kwa sasa hana akaunti ya Instagram.

Showbiz: Mtoto wenu anaishi wapi na nani?

Nuh: Anaishi Ilala kwa mama yangu mzazi.

Showbiz: Nawal akiomba mrudiane, inawezekana?

Nuh: Hapana, sihitaji kabisa mwanamke kwa sasa.

Showbiz: Kwa nini?

Nuh: Basi tu, sina mawazo hayo.

Showbiz: Una bifu na Shilole?

Nuh: Hapana.

Showbiz: Mbona ulisema huwezi kununua bidhaa zake za pilipili?

Nuh: (Anatabasamu) Kwa sababu hata mama yangu anauza pilipili mbilimbi. Ni vizuri zaidi nikimuungisha mama yangu.

Showbiz: Uliwahi kubadili dini kipindi upo na Nawal, lakini baada yakuachana naye ukarudi tena kuwa Mkristo, je, akitokea mwanamke mwingine Muislam ukataka kumuoa unaweza kubadili dini tena?

Nuh: Hapana, ila hizi stori sitaki tena kuzizungumzia.

Showbiz: Ukitaka kuoa, utapenda mwanamke mwenye sifa zipi?

Nuh: Yeyote ambaye Mungu atakuwa amenipangia nioe.

Showbiz: Mara nyingi umekuwa ukisema utatambulisha wasanii kutoka kwenye studio yako ya Last Born, lakini bado, lini hili litatokea?

Nuh: Ni kweli nimekuwa nikisema hivyo na sitekelezi. Lakini kwa sasa tupo Zanzibar na msanii wangu aitwaye Bi Aisha, tumekuja kushuti video ya wimbo wangu na wimbo wake na baada ya kumaliza hii shughuli nitamtambulisha watu wamfahamu.

Showbiz: Ni wasanii gani wamewahi kurekodi kwenye studio yako?

Nuh: Wapo wasanii wengi, kwa mfano Alikiba alirekodi wimbo wake ule uliotumika kwenye kampeni Kenya, Matonya, na wasanii wengine wengi.

Showbiz: Una jambo gani la kumalizia?

Nuh: Ninawapenda mashabiki zangu na wazidi kunipa sapoti.

MEMORISE RICHARD

Comments are closed.