The House of Favourite Newspapers

Nunua Bidhaa Mtandaoni Kupitia Mastercard na M-Pesa

WANUNUZI  wa bidhaa mtandaoni huenda sasa wakapata machaguo zaidi ya ulipaji baada ya shirika la huduma za kifedha la Mastercard na Vodacom Tanzania PLC kuanzisha mfumo wa malipo wa ‘virtual card’ unaoruhusu kulipia huduma au bidhaa popote ulimwenguni kwa kutumia simu ya mkononi.

 

Watumiaji wa Vodacom M-Pesa wana uwezo wa kulipia bidhaa au huduma zozote ulimwenguni ambazo zinaruhusu malipo mtandaoni kwa kupitia mfumo wa ulipiaji wa Mastercard kama tovuti ya Amazon au eBay.

 

Ili kulipia, watumiaji hao wa M-Pesa watalazimika kutengeneza kadi hiyo na kupata taarifa za siri kuhusu Mastercard kupitia huduma hiyo ya kadi inayopatikana kwa sasa kupitia mfumo (menu) ya M-Pesa. Vodacom imeeleza kuwa itawezesha mfumo huo wa malipo katika programu ya M-Pesa (app) kwa wale wanaotumia simu janja (smartphone).

Kupitia M-pesa, yenye wateja milioni 8.2 na wakala zaidi ya 100,000, wanunuzi wa bidhaa na huduma mtandaoni wanaweza kufanya malipo hayo hadi kwenye tovuti za kimataifa kupitia mfumo huo mpya ulioundwa kwa kushirikiana na benki ya biashara ya BancABC.

Comments are closed.