The House of Favourite Newspapers

Kanye West Kukutana Tena na Donald Trump

Image result for kanye west and donald trump

RAPA Kanye West ameonekana kukosolewa na mashabiki siku kadhaa zilizopita baada ya kuibuka kwenye kipindi cha Saturday Night Live akiwa amevaa kofia iliyoandikwa ‘Make American Great Again (MAGA)’ ambayo ni kauli mbiu ya Donald Trump.

Mashabiki walihoji na kusema kuwa Kanye anam-support  Rais Donald Trump na kauli hiyo inayoonekana kuwa ni ya uonevu kwa Wamarekani.  Kwa mujibu wa mtandao wa New York Times,  rapa huyo atakutana na Rais Trump Alhamisi ya Oktoba 11, 2018.

Kanye  amewahi kuripotiwa kula chakula cha mchana  na Rais Trump yakiwemo mazungumzo kuhusiana na mchango wa kuwapa ajira vijana wa Chicago.   Iliwahi kusemekana pia kuwa Kanye alizungumzia ishu ya kugombea urais wa Marekani mwaka 2020.

Comments are closed.