The House of Favourite Newspapers

Dhamana: Mdee, Bulaya, Msigwa, Heche Wapeta Kortini – Video

MAHAKAMA ya ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 20, 2019 imetoa uamuzi kuwa wabunge wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao ni miongoni mwa watuhumiwa wa kesi ya uchochezi, waendelee na dhamana yao.

 

Wabunge hao ni John Heche (Tarime Vijijini), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao wamefika mahakamani hapo leo wakitokea katika kituo cha polisi cha  Oster Bay baada ya kujisalimisha kufuatia amri ya mahakama ya kuamuru wakamatwe kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana yao.

 

Washtakiwa wote wanne jana walitoa sababu za kutokufika mahakamani siku ya Novemba 15 mwaka huu saa tatu asubuhi kama mahakama ilivyokuwa imepanga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.  Kesi imeahirishwa hadi Novemba 26, mwaka huu.

 

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko.

 

Katika kesi hiyo Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 13, yakiwemo ya kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.  Maandamano hayo yalisababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Comments are closed.