The House of Favourite Newspapers

OFM YAFUMUA SOKO LA GONGO DAR!

WAKATI Rais Dk. John Magufuli akisisitiza juu ya Watanzania kufanya kazi kwa bidii, bado kuna baadhi ya watu wanaonekana kuweka ‘pamba’ masikioni, wanakunywa gongo muda wa kazi, kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kinawafichua.  

NI MTAA WA MAKONGO Kitengo cha OFM kimefichua ‘soko’ maarufu la kuuza gongo lililopo Mtaa wa Makongo jijini Dar, ambapo wateja wa pombe hiyo ya kienyeji wamepaita Sheli.

“Yaani Sheli ukifika gongo muda wowote unaipata. Iwe asubuhi, mchana au jioni mzigo unaupata, pale ni kama soko kabisa maana mbali na gongo, ukifika unaweza kupata aina mbalimbali ya pombe za kienyeji muda wote,” chanzo kiliwaeleza OFM na kuongeza:

 

“Kwa kweli eneo hilo ni tatizo, ni eneo la makazi ya watu, gongo huuzwa kuanzia saa mbili asubuhi ikiwa ni eneo ambalo watoto wamekuwa wakishuhudia vitendo vichafu vikiendelea ikiwemo kupigana na kutukanana, kwa kweli ni tatizo.” Baada ya kupata habari hiyo, makachero wa OFM walifika na kujiridhisha kweli pombe mbalimbali za kienyeji zinauzwa muda wa kazi na watu wakiingia na kutoka.

 

OFM walipofanikiwa kupiga picha za eneo la tukio, walimtafuta mjumbe wa eneo hilo ili kumsikia anazungumziaje tatizo hilo lililopo mtaani kwake. Mjumbe wa mtaa huo wa Makongo, Kata ya Makongo Juu, Said Mfaume Manjoti kwanza alikiri kuwepo kwa soko hilo la pombe na kudai kuwa, ameshapeleka malalamiko kwenye ofisi ya mtendaji.

“Mimi nimeshapiga kelele sana kuhusu eneo hilo na hata hawana leseni lakini ndio hivyo tena, wanaendelea na wanakunywa pale kuanzia saa mbili asubuhi na pombe zote za kienyeji zinauzwa pale, linaendeshwa na mtoto wa marehemu Mathias Lucas, anayeitwa Andolick na walevi wengi saa mbili asubuhi wanakunywa gongo ila ndio hivyo tena wameshindikana,” alisema mjumbe huyo.

 

Mjumbe huyo aliiomba Serikali ngazi za juu imsaidie ili ikiwezekana eneo hilo lifungiwe. “Naomba kama inawezekana Serikali ilisimamie hili kwa sababu hata kaka yake alishamkanya Andolick) lakini anaona kama anamfanyia fitina asiendelee na biashara na kiukweli mimi nimeshapiga marufuku kuja kwangu kushitaki kwa sababu utakuta wanakuja kukuamsha saa nane usiku wamepigana na wanataka barua waende polisi wakiwa wamelewa kwa hiyo mimi sihitaji usumbufu,” alisema Said.

Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mtaani hapo, Pius Prosper anayesimamia usalama wa eneo hilo alisema wameshachukua hatua kwa wahusika lakini wahusika ni wakaidi.

 

“Wauzaji na mmiliki tulishawakamata na kuwapa onyo kali lakini bado wanaendelea kuuza. Na baada ya hapo tuliwapeleka polisi na waliwekwa ndani lakini ndio hivyo tukiwa tunaenda eneo lile wakituona tu huwa wanakimbia,” alisema Pius.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Murilo Jumanne Murilo alipoulizwa kuhusu uwepo soko hilo la pombe alisema: “Halijanifikia suala hilo mezani kwangu, lakini kwa kuwa umeniambia, nitafuatilia

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko

Comments are closed.