The House of Favourite Newspapers

Okwi: Nashindwa Kufunga Mkoani

0
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiongea jambo.

MSHAMBULIAJI matata wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa licha ya kutamani kufunga kwenye michezo ya timu hiyo ya mikoani lakini anashangazwa na ubutu ambao unamtokea.

 

Licha ya Okwi kufunga mabao nane kwenye ligi hadi sasa lakini ameshindwa kufunga bao hata moja kwenye mechi za timu hiyo ikiwa inacheza kwenye viwanja vya ugenini hasa mikoani.

 

Okwi aliyekuwa SC Villa ya Uganda kabla ya kuja Simba msimu huu ameliambia Championi Jumatano kuwa, hali hiyo kwa sasa anamuachia Mungu kama atamjalia kufunga mikoani basi atafunga lakini kwa upande wake lengo lake la kwanza ni kufunga kila mchezo.

 

“Kiukweli napenda kufunga katika kila mchezo wetu iwe ugenini au tunacheza nyumbani kwa sababu hayo ndiyo malengo yangu niliyojiwekea kwa sababu nataka kuipa timu ubingwa na hatuwezi kufanya hivyo bila ya kushinda kila mechi.

“Lakini nashangaa ninapopanga kufunga mikoani mambo huenda kombo na kujikuta sifungi, lakini yote kwa yote sasa namuachia Mungu kwani yeye ndiye anapanga kila kitu juu ya mabao, lakini mimi nitaendelea kujituma kuhakikisha nafunga,” alisema Okwi.

Leave A Reply