The House of Favourite Newspapers

OKWI WA 2011/12 Vs 2017/18

MARA ya mwisho fu­raha ya Wanasimba kuweza kutwaa ub­ingwa ilikuwa ni msimu wa 2011/12 na baada ya hapo wakakaa miaka mitano bila kuonja raha ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara kabla ya msimu huu wa 2017/18 kuupata.

Timu hiyo imetwaa ubingwa wake ukiwa ni wa 19 tangu ligi hiyo ilivyoanzishwa mwaka 1965 huku wapinzani wao, Yanga wakitwaa mara 27.

Mshambuliaji Em­manuel Okwi ni mmoja kati ya wachezaji waliokuwa chachu ya mafanikio ya ubingwa katika msimu wa mwaka 2011/12 na msimu huu akaonyesha tena kiu ya kuutwaa.

Okwi, ambaye ni raia wa Uganda, ni mmoja wa wachezaji ambao unaweza kuwataja kwenye listi ya wale waliosaidia mafanikio hayo ya Simba kwa zaidi ya 50% kwani licha ya kufun­ga mabao 20 pia ameweka rekodi mbalimbali ndani ya kikosi hicho.

Tuungane kuzitazama baadhi ya rekodi ambazo zimewekwa na straika huyo aliyejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea SC Villa ya Uganda.

MABAO

Msimu wa 2011/12 ambao Simba walikuwa machampioni wa ligi kuu, Okwi alifunga mabao 12 nyu­ma ya kinara John Bocco aliyefun­ga 19 ambaye wakati huo alikuwa Azam FC na sasa wanacheza wote Msimbazi. Lakini msimu huu Okwi yupo juu na mabao 20 na Bocco yupo nafasi ya pili akiwa nayo 14.

Msimu huo Okwi ndiye ali­yekuwa kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba na kuisaidia kut­waa ubingwa.

MABAO NJE YA DAR

Msimu wa 2011/12, Simba licha ya kutwaa ubingwa lakini Okwi katika ufungaji wake wa mabao hakufanikiwa kufunga bao lolote nje ya Dar kati ya yale 12 na ku­weza kuweka rekodi yake.

Msimu huu mpaka sasa ame­funga mabao 20 na kati ya hayo amefanikiwa kufunga mabao mawili nje ya Dar ambayo alifun­ga dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyan­ga na Mtibwa Sugar pale Jamhuri, Morogoro.

HAT TRICK

Kipindi cha mwisho kutwaa ub­ingwa yaani msimu wa 2011/12, Okwi hakuweza kupiga ‘hat trick’ yoyote katika mabao yake 12, lakini msimu huu katika mabao yake 20 amefanikiwa kupiga moja dhidi ya Ruvu Shooting ka­tika ushindi wa mabao 7-0 ambapo yeye alifun­ga manne ‘Quadruples’.

A V U N J A REKODI YA TANO

Straika huyu am­baye pia hupende­lea kunyoa kiduku,

amefanikiwa kuandika rekodi ya kipekee kwa upande wa mabao mara ya mwisho Simba ilipochukua ubingwa mpaka msimu huu.

Msimu wa 2011/12 Bocco ali­funga mabao 19, rekodi hiyo Okwi ameivunja na hata za misimu iliyo­fuata amezivuja isipokuwa ile ya Amissi Tambwe aliyotupia mabao 21 msimu wa 2015/16.

MKALI KWA MAAFANDE

Katika mabao ambayo alifunga katika msimu wa 2011, Okwi alizifunga timu za jeshi za JKT Oljoro na Ruvu Shooting ma­bao manne lakini safari hii kupitia timu hizo za jeshi alifunga mabao ma­tano. Dhidi ya Ruvu alipiga manne na ak­ifunga bao moja dhidi ya Tanzania Prisons.

MCHEZAJI BORA WA MWEZI

Msimu wa 2011/12 hakukuwa na tuzo ya wachezaji bora wa mwezi la­kini msimu huu alifungua pazia kwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Ago­sti, baadaye akashinda tena Aprili.

MECHI

Katika mechi 27 ambazo Sim­ba imecheza mpaka sasa Okwi am e c h eza 22, aliko­sa mechi dhidi ya Mbeya City, Prisons, Azam FC, Ndanda na Kagera zote za mzunguko wa kwanza. Mpaka sasa Simba hai­japoteza mchezo wowote na imekusanya p o i n t i 65 ka­tika mich­ezo 27, msimu wa 2 0 1 1 / 1 2 walip o te za m i c h e z o miwili pekee mpaka ligi i n amaliz i k a, u k i w e m o mchezo ule dhidi ya Yanga ambapo wali­fungwa bao 1-0 na wakalipiza 5-0 na wakitwaa ubingwa kwa pointi 62 katika michezo 26.

REKODI YA UB­INGWA

Okwi anaweka rekodi kwa kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu akiwa Simba ubingwa ule wa kwanza ulikuwa wa mwaka 2009/10 ambapo Simba ilitwaa bila kupoteza na ika­fanikiwa kuutwaa tena 2011/12 na 2017/18.

Makala – Bongo, 

MARTHA MBOMA, Dar es Salaam

Comments are closed.