The House of Favourite Newspapers

Olimpiki Yajadili Kuahirisha Michuano ya Japan

0

 

KAMATI ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesema inaangalia uwezekano wa kuahirisha Michuano ya Olimpiki mwaka 2020 kutokana na mlipuko wa #CoronaVirus, ambapo itatoa uamuzi ndani ya wiki nne.

 

Taarifa iliyotolewa na IOC imesema Bodi ya Utendaji imeanza taratibu mpya za kuandaa mpango wa mazingira maalum ambao utaboresha mipango iliyokuwepo awali.

 

Imesema licha ya hali mbaya duniani kote, kufuta kabisa michuano hiyo sio ajenda mojawapo, na kwamba wanaweza kufikiria kupunguza idadi ya michezo na kubadili tarehe.

 

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema kufuta michuano hiyo iliyopangwa kuanza Julai 24 mwaka huu jijini Tokyo haiwezekani.

 

Hata hivyo, ameweka wazi kuwa kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa Olimpiki kuahirishwa ikiwa watashindwa kuiandaa kikamilifu.

 

Aidha, Canada imetangaza kujitoa katika michuano hiyo na kuitaka IOC kuahirisha Olimpiki kwa mwaka mmoja. Australia nayo imewataka wanariadha kujiandaa na michuano ya mwaka 2021 badala ya ile ya mwaka huu.

 

Leave A Reply