The House of Favourite Newspapers

Omog Awazuga Yanga Kwa Okwi

0
Kocha wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog.

KOCHA wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog hakuweza kumtumia mshambuliaji wake raia wa Uganda, Emmanuel Okwi katika michezo ya kirafiki visiwani Zanzibar kwa madai ya kuwa ni majeruhi lakini amesisitiza kuwa lazima atacheza katika mchezo wa leo Jumatano dhidi ya Yanga.

 

Timu hizo zinatarajia kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, baada kumaliza kambi ya wiki moja Zanzibar kwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ambapo katika mchezo wa kwanza walicheza dhidi ya Mlandege na kutoka suluhu kabla ya kuifunga Gulioni mabao mabao 5-0.

Raia wa Uganda, Emmanuel Okwi.

Okwi ambaye amefanya mazoezi na timu hiyo kwa siku zote kwenye Uwanja wa Ngome uliopo Fuoni, Wilaya ya Mjini Magharibi na kwenye Uwanja wa Amaan, hakuweza kucheza michezo yote waliyocheza kisiwani humo huku ikidaiwa kuwa Omog amefanya hivyo ili kuwapoteza Yanga waamini kuwa ameumia sana.

 

“Kwanza sikuhitaji kabisa kuona akipata majeraha mengine katika hizi mechi ambazo tumecheza kwa sababu tuna mechi kubwa sana dhidi ya Yanga ndiyo maana nilichokifanya ni kuhakikisha anafanya mazoezi kwa asilimia zote ili aweze kucheza mchezo huo kuliko hizi za kujipima.

 

“Unajua hilo limetokana na kupata majeraha ya misuli na tatizo la nyama za paja ingawa halikuwa linaweza kumzuia kucheza, hivyo nilichokifanya ni kutoa muda wa kutosha kwake ili aweze kuwa sawa kwani nategemea atacheza hiyo mechi kwa asilimia zote,” alisema Omog.

Stori: Ibrahim Mussa, Championi Jumatano

Leave A Reply