The House of Favourite Newspapers

Oryx Gas Tanzania, Benki Ya NMB Kushirikiana Kusambaza Mitungi Gesi Kote Nchini

0
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB Filbert Mponzi (kulia)wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati katika kuhakikisha ufumbuzi wa nishati safi ya kupikia kupatikana kwa kila mtu.Ushirikiano huo umefikiwa leo Novemba 27,2023 jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam 27 Novemba 2023: KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania pamoja na Benki NMB wamesaini hati ya ushirikiano wa usambazaji gesi wenye lengo wa kimkakati katika kuhakikisha ufumbuzi wa nishati safi ya kupikia kupatikana kwa kila mtu.

Kupitia ushirikiano huo ulioingiwa leo Novemba 27, 2023 jijini Dar es Salaam, utawezesha wananchi kununua mitungi ya gesi ya Oryx kupitia Benki ya NMB sambamba na punguzo la bei kwa mitungi ya gesi hiyo lengo kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanatumia nishati safi ya kupikia.

Akizungumza wakati wa kusaini hati ya ushirikiano Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania, Benoit Araman amesema kupitia mtandao wao wa usambazaji pamoja na uhamasishaji mkubwa kutoka kwa NMB utaleta hatua nyingine muhimu kwa Watanzania kupata bidhaa zetu kwa urahisi, haraka na ufanisi.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB Filbert Mponzi (kulia) wakionesha hati za makubaliano hayo baada ya kutiliana saini.

Kwa miaka mingi Oryx Gas Tanzania Ltd imekuwa kampuni ongozi katika kukuza matumizi ya Gesi nchini na hivi karibuni kuanzia mwaka 2021 wamekuwa wakiratibu juhudi za kuunga mkono ajenda ya Serikali iliyoidhinishwa na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan aliyetoa maelekezo kuwa ifikapo mwaka 2032, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

“Leo tunashuhudia mdau mwingine (NMB) akiungana nasi katika kufanikisha adhma hii ya Rais wetu na ndoto ya Watanzania wengi. Wasambazaji wetu na maduka ya Oryx pekee yaani exclusives hops yaliyopo nchi nzima yatakuwa tayari kuwahudumia wateja wote wa NMB ambao watakuwa wakitumia Kadi zao za Benki au huduma nyingine za kufanya malipo kulipia Gesi.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman akizungumza kwenye hafla hiyo.

“Oryx Gas Tanzania iko katika safari kubwa ya upanuzi wa kueneza nishati safi ya kupikia nchini kote tangu. Kupitia mipango hii, Oryx Gas inataka kutokomeza matumizi ya nishati mbaya ya kupikia ambayo si tu hatari kwa afya zetu bali pia kwa mazingira yetu.

“Kupitia ushirikiano huu wasambazaji wakuu wa Oryx Gas na maduka ya Oryx pekee yataweza kutoa huduma za kitaalamu na kidijitali zaidi kwa wateja wao. Oryx Energies ni mojawapo ya watoa huduma huru wakubwa na wa muda mrefu zaidi barani Afrika wa bidhaa na huduma za mafuta na gesi.

“Biashara yetu iliyoanzishwa tangu 1999 nchini Tanzania, inaendeshwa kupitia kampuni kuu nne nchini Tanzania.Pia Kampuni ya Oryx Oil Company Limited, inayojishughulisha na uhifadhi na usambazaji wa mafuta, ikiwa na uwepo mkubwa katika sehemu ya reja reja na, zaidi ya yote, kama muuzaji chaguo bora kwa sekta ya viwanda na madini. Inavituo57 vya reja reja kufikia leo na inaendelea kukua, ” amesema Araman.

Wakibadilisha mawazo baada ya kuingia makubaliano hayo.

Ameongeza Oryx Services and Specialties Ltd, iliyobobea katika uchanganyaji wa aina kamili za vilainishi vya chapa ya Oryx Energies, pamoja na makampuni mengine ya uuzaji wa mafuta kupitia kiwanda chetu cha uchanganyaji cha Dar es Salaam.

Amesisitiza Oryx Gas Tanzania Ltd imejikita katika uhifadhi, ujazaji na usambazaji wa LPG katika mitungi na watumiaji wakubwa kama viwanda na hotel ( yaani Bulk consumer). Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd inaongoza katika soko lisilopingika la gesi ya Liquefied Petroleum Gas (LPG) nchini Tanzania.

Baadhi ya wafanyakazi wa Oryx na NMB kwenye hafla hiyo.

“Oryx Gas ni mshirika mkuu anayechaguliwa kwa usambazaji wa LPG kwa wateja wa rejareja, wa kibiashara na wa viwandani kote nchini na itaendelea kuwekeza na kupanua uwepo wa huduma zake na ushirikiano katika maeneo mengi zaidi nchini Tanzania kwa kuwa tunaamini aina hizi za ubia sio tu zinachangia ukuaji wa kampuni…

” Hata hivyo, hufanya kama chachu katika kuleta mageuzi ya utoaji huduma ndani ya tasnia. Zaidi ya hayo, huongeza mapato kwa serikali yetu, kuongeza nafasi Zaidi za ajira.Kwa washirika wetu, NMB, tunatarajia kufanya kazi pamoja, kukua pamoja na kuhakikisha wateja wetu wanafurahia vyema kutoka kwetu sote na huduma bora wanazostahili.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi , amesema malibaliano hayo yanaendana na mkakati wa benki hiyo wa kutunza mazingira.

Amesema mapema mwaka huu walizindua mkakati wa kupanda miti bilioni moja nchi nzima ambao utekelezaji wake unaendelea lengo ni kuhakikisha mazingira tanatunzwa kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Mponzi amesema bodi ya NMB iliidhinisha sh. bilioni mbili katika bajeti ya mwaka huu wa fedha ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika shughuli mbalimbali za kutunza mazingira.

“Tunawahakikishia Watanzania kuwa tumedhamiria kuimarisha utunzaji wa mazingira, kupotia makubaliano haya tutatoa ofa ya punguzo la gharama za gesi kwa mitungi ya viwango mbalimbali inayouzwa za Oryx Gas Tanzania.

Mmoja wananchi mkazi wa Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam, Mwanahawa Mfaume, amepongeza makubaliano hayo kwani yatawasaidia kupunguza gaharama za gesi.

“Iwapo mitungi ya gesi itapatikana kwa bei himilivu na kujazwa kwa gaharama nafuu, itawahamasisha wananchi wengi kutumia huduma hiyo na kuonfokana na matumizi ya kuni na mkaa.”

Leave A Reply