The House of Favourite Newspapers

Pam D Roma wazua utata ATM

0

15. Mwana Hip Pop kutoka Tanga Roma Mkatoriki ni moja kati ya watu waliofanya poa kwenye jukwaa hiloMAYASA MARIWATA

WASANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ na Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ hivi karibuni walizua utata baada ya kuonekana wakiwa wamegandana kwa mapozi ya kimahaba kwenye mashine ya kuweka na kutolea fedha ‘ATM’ maeneo ya Makumbusho jijini Dar.

PAM D (32)Kwa mujibu wa sosi aliwashuhudia, wawili hao walikuwa wakienda ATM kutoa hela wakiwa wameshikana mikono kwa huba na mahaba tele bila kuhofia macho ya watu jambo lililoacha viulizo sababu ya wao kufanya hivyo huku Roma akiwa ni mume wa mtu na ndoa yake ikiwa bado changa.

Showbiz Xtra ilimvutia waya Roma kuhusiana na ishu hiyo ambapo alijibu kwa kifupi tu kuwa mwanadada huyo ni rafiki yake wa karibu tu na alipotafutwa Pam anayebamba na Ngoma ya Nipe Nono naye alifunguka kuwa;

“Sisi si wapenzi ila tumezoeana sana na mke wake ananijua, kifupi ni mambo ya Kizungu tu.”

Leave A Reply