The House of Favourite Newspapers

Pambano la Mayweather, Logan Hakuna Mshindi

0

PAMBANO kati ya  Floyd Mayweather na Logan Paul 26   limemaliza roundi zote nane na hakuna mshindi, kwa kuwa pambano hilo lilikuwa la hisani  (exhibition match).

 

Baada ya Pambano hilo ambalo limepigwa usiku wa kuamkia leo Juni 7, Flyod ameseam huenda ikiwa ni mara ya mwisho kuonekana kwenye ulingo wa masumbwi hiyo ikiwa inazima ndoto za wapenda ngumi kuona anarudiana na   Conor McGregor.

 

Sheria zake zilikuwa tofauti kidogo Roundi zilikuwa za dakika tatu, hakuna mshindi atakaetangazwa na pambano hilo lilikuwa halina  Majaji.

 

Inasemekana Mayweather ambaye kwa sasa ana miaka 44 amevuta mpunga mrefu sana kwenye pambano hilo.

Leave A Reply