The House of Favourite Newspapers

Wiki Sita Kabla ya Usajili…Panga Limeanza Yanga SC

KIWANGO cha Yanga hususani kwa mastaa wapya waliosajiliwa kimewatia shaka mashabiki ambao wameshinikiza Kocha Mkuu Mwinyi Zahera aondoke na yafanyike mabadiliko makubwa kwa kupiga chini wachezaji mizigo.

 

Mashabiki hao ambao leo saa 2 usiku watakuwa kwenye runinga wakiangalia mechi ya Yanga na Pyramids, uongozi umepania kuwafanyia sapraizi kwenye usajili wa dirisha dogo kabla ya mechi ya watani wa Januari 4 kwenye Uwanja wa Taifa.

 

Mmoja wa viongozi wa Yanga, ameidokeza Spoti Xtra kwamba wameshaweka sawa mambo mengi ya kiutendaji sasa wanataka kutumia dirisha dogo kutengeneza timu itakayoleta mshtuko uwanjani tofauti na hali ilivyo sasa. Kitaifa na kimataifa Yanga imekuwa na tatizo kwenye ushambuliaji, katika mechi tano za kimataifa imefunga mabao matano pekee huku ikiruhusu kufungwa mabao sita.

Licha ya usajili wao wa mastaa 15, bado wameshindwa kufurukuta ambao ni Lamine Moro, Seleman Moustapha, David Molinga, Farouk Shikhalo, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Juma Balinya, Maybin Kalengo na Sadney Urkhob.

 

Ali Ali, Ally Sonso, Mapinduzi Balama, Metacha Mnata,Abdulaziz Makame na Mwarami Issa ambao ni wazawa bado hakuna aliyeoonyesha makali yake zaidi ya Molinga tu aliyefunga
mabao mawili kwenye ligi kwa upande wa wageni.

 

Balinya na Urkhob wametupia bao mojamoja lakini hawana uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza mpaka sasa jambo ambalo limekuwa likiwatia hasira mashabiki ingawa Zahera amewapuuza kwa madai kuwa amezoea hali hizo Afrika. Habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kwamba wameweka mkakati mkubwa wa kufanya mabadiliko baada ya Shirikisho la Soka la Tanzania kutangaza kwamba dirisha dogo linafunguliwa Desemba 16.

 

Hiyo inamaanisha kwamba zimebaki wiki sita sawa na siku 43 kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Desemba 16 na litafungwa 15 Januari. Mmoja wa viongozi mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Yanga alisema kwamba baada ya mchezo wa leo dhidi ya Pyramids kwa matokeo yoyote, watataka maelezo ya kina kutoka kwa Zahera na kupata uelekeo wa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya wiki sita zijazo.

 

“Kuna viwango vya wachezaji hatuvielewi mpaka sasa, tunafi kiria kufanya mabadiliko makubwa na kuongeza sura chache za kazi za kutubeba kwenye Ligi na vilevile kuachana na wachezaji ambao wanaigharimu klabu na hawafanyi kazi inayoonekana, haswa hawa wageni,”alisema kiongozi huyo.

 

Tangu msimu huu uanze safu mbalimbali ndani ya timu hiyo zimefanya yafuatayo; FOWADI Mabao 10 ambayo wamefunga kwenye jumla ya mechi tisa yanawasikitisha viongozi na mashabiki kwani inaonyesha tatizo la ubutu wa safu ya ushambuliaji ni kubwa tofauti na Simba ambao wamefunga mabao 12 kwenye mechi 7 za ligi.

 

Zahera amesisitiza kwamba baadhi ya wachezaji wake akiwemo Juma Balinya, Urikhob, Kalengo na Sibomana walikumbana na hali fulani zinazoashiria ushirika wakati wakiwa kambini jambo ambalo limewatia uoga. Lakini viongozi wamehitaji maelezo ya kina ya Urikhob na Kalengo kabla ya kufanya maamuzi.

 

ULINZI Hapa kichwa cha Zahera lazima kipasuke kidogo huku mkwanja utapaswa utemwe kutokana na ukweli kwamba hakuna mbadala wa safu ya ulinzi ambayo kwa beki wa kati inamtegemea Kelvin Yondani, Lamine Moro na mbadala wao akiwa ni Ally Sonso ambaye bado hajaweza kufi ti vizuri.

 

Beki wa kulia yupo Juma Abdul, Paul Godfrey ambao hawa wakiumwa imekuwa ikimpa shida Zahera kwa kumchezesha Ali Ali pamoja na Mapinduzi Balama. VIUNGO Kiufundi pameonekana
Kitaifa na kimataifa Yanga imekuwa na tatizo kwenye ya Shirikisho la Soka la Tanzania kutangaza kwamba wamehitaji maelezo ya maelezo ya kina ya Urikhob na Kalengo
hakuna tatizo kubwa yupo Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mapinduzi Balama, Papy Tshishimbi, Mohamed Banka, Abdulaziz Makame.

 

WATAKAOPIGWA CHINI Mpaka sasa upepo haujawa mzuri kwa Maybin Kalengo, Issa Bigirimana na Seleman Mostapha hatma yao ipo kwa Zahera huku kwa wazawa Ali Ali akitazamwa kwa ukaribu kutokana na mwenendo wake kuwa ni maji kupwa na kujaa.

 

Lakini viongozi wamesisitiza kwamba ndani ya mwezi mmoja wa usajili mdogo
yatafanyika mabadiliko makubwa na zitaingia sura za kushtua Yanga huku mastaa kadhaa pia wakienda na maji kutegemeana na maelezo ya Zahera ambaye nae ajira yake i po shakani. Habari kutoka ndani ya uongozi zinasema kwamba kama watakubaliana kufanya mabadiliko makubwa kwenye benchi la ufundi kwa kumtoa Zahera, idadi ya wachezaji watakaokwenda na maji huenda ikaongezeka zaidi.

Comments are closed.