The House of Favourite Newspapers

Papa Francis: Wanaotoa Mimba ni Wauaji

0

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema kuwa utoaji mimba ni “mauaji”, hata muda mfupi baada ya kupata ujauzito.

 

Hatahivyo alionekana kuwakosoa baadhi ya Maaskofu wa Kanisa katoliki wa Marekani kwa kushugulikia msimamo wa Rais wa Marekani Joe Biden wa kuunga mkono utoaji mimba kwa njia ya kisiasa badala ya njia ya kitume. Papa Francis aliyasema hayo ndani ya ndege alipokuwa safarini kutoka nchini Slovakia jana Jumatano.

 

Akizungumza kuhusu mjadala wa Maaskofu wa Marekani, kuhusu iwapo Rais Biden, ambaye ni Mkatoliki anapaswa kukataliwa kushiriki Komuniyo(Ekaristi), kwasababu anaunga mkono haki ya wanawake kuchagua kutoa mimba, hata kama yeye anapinga hilo, Papa Francis alisema:

 

“Sitamzuwia mtu yeyote kupokea Komuniyo, lakini sikuwahi kufahamu kwamba nina mtu mbele yangu kama kama wewe unayemuelezea, hilo ni ukweli ,” alisema, bila kufafanua zaidi.

 

“Komuniyo sio tuzo kwa watu wasio na kasoro ya dhambi … Komunio ni zawadi, uwepo wa Yesu na kanisa lake. Utoaji mimba ni mauaji… Wale wanaotoa mimba wanaua ,” alisema Papa Francis.

 

“Katika wiki ya tatu baada ya mwanamke kupata mimba, mara nyingi hata wakati mama hajatambua (kuwa ana unjauzito), viungo vyote vya mwili tayari huwa vimeanza kukua. Ni maisha ya binadamu.Kweli!. Na haya maisha ya binadamu yanapaswa kuheshimiwa. Ni wazi kabisa. Kisayansi, ni maisha ya binadamu,” alisema Papa Francis.

 

Mwezi Juni mwaka jana Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Roma nchini Marekani walipigia kura taarifa ya muswada juu ya ushiriki wa Komuniyo ambao unaweza kuwazuwia wanasiasa kushiriki Komuniyo akiwemo Rais Biden.

Leave A Reply