The House of Favourite Newspapers

PSG Imevutiwa na Mpango wa Kuinasa Saini ya Marcus Rashford

0
Marcus Rashford

KLABU ya Paris Saint- Germain ya nchini Ufaransa inaangalia uwezekano wa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford ili kwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo tayari ina nyota kadhaa akiwemo Kylian Mbappe, Neymar Jr pamoja na Lionel Messi.

 

 

Kocha wa PSG Christophe Galtier amekiri kuwa anataka mshambuliaji mpya.

Christopher Galtier Kocha Mkuu wa Klabu ya Paris Saint Germain

Mkufunzi wa PSG Christopher Galtier, ambaye aliondoka Nice kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino katika dimba la Parc des Princes msimu huu wa joto, anasema anataka kusajili mshambuliaji mpya mwezi huu.

 

“Ndiyo, tunatamani ujio wa mshambuliaji mpya,” Galtier alikiri. “Narudia tena, kwa kalenda yenye shughuli nyingi hadi Novemba 13, pamoja na Kombe la Dunia, ni wazi tunatamani ujio huu.” amesema Galtier.

Galtier anamtaka Rashford kwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu yake

Manchester United wametulia kuhusu hali hiyo kwa sababu Rashford amejitolea kuitumikia klabu hiyo huku mshambuliaji huyo akiwa amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake.

Leave A Reply