The House of Favourite Newspapers

Pasaka; Lulu, Akina Mbowe Watikisa Segerea

Wakati Wakristo wote na wasio Wakristo duniani wakishere­hekea Sikukuu ya Pasaka juzi na jana, muigizaji wa sinema nchini, Elezabeth Michael ‘Lulu’ na viongozi wa Chadema walioko Gereza la Segerea jijini Dar, wametikisa viunga vya gereza hilo kuto­kana na uwepo wao wakati wa sikukuu.

 

Lulu na Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine watano wa Chadema wali­tikisa juzi Jumapili baada ya watu mbalimbali walipokuwa wakitaka kwenda kula nao Pasaka lakini ghafla ku­kasambaa ujumbe mitandao­ni, uliokuwa ukieleza kuwa hairuhusiwi kuwaona maha­busu siku hizo.

“Yani huku gerezani kila mtu anajadili tu kuhusu kula sikukuu na viongozi wa Chadema na huyu muigizaji Lulu.

 

“Watu wamesambaziana ujumbe mitandaoni kuwa tumewazuia watu kuja huku gerezani kuja kuona jamaa zao kitu ambacho si cha kweli. Sasa wamefanya watu wengi wawajadili sana hawa huku wengi wakishindwa kuja kwa kuogopa kwamba hawataruhusiwa,” alisema askari mmoja wa magerereza aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji gazeti hili lilipotembelea gereza hilo.

Hata hivyo, ujumbe huo ulibainika kuwa haukuwa na ukweli wowote kwani baadhi ya viongozi wa Chadema ak­iwemo Joseph Haule ‘Profesa Jay’, Mbunge wa Mikumi, wa­liruhusiwa kwenda kuwaona.

 

Akizungumza na Uwazi mara baada ya kutoka gerezani humo, Profesa Jay alisema Mbowe amempa ujumbe kwamba kinacho­tokea sasa hivi ni harakati za ukombozi.

Alisema matendo kama ya viongozi kuwekwa mahabu­su, watu kupotea, kuvunjwa miguu na kuteswa ni jambo la kawaida katika kuelekea kwenye ukombozi kama Musa alivyowakomboa wana wa Israeli.

 

Lulu.

 

Katika hatua nyingine, askari magereza aliyezun­gumza na Uwazi, alisema licha ya viongozi hao kuwa gumzo siku hiyo ya Pasaka, bado ndugu na jamaa wali­weza kuwatembelea ndugu zao waliopo gerezani kwa makosa mbalimbali.

“Gumzo limekuwa kubwa sana kuhusu hawa kina Lulu na akina Mbowe lakini kimsingi sisi hatukuzuia watu kama walivyotumiana jumbe mitandaoni,” alisema askari huyo.

 

Mbali na Mbowe, vion­gozi wa Chadema wengine waliowekwa gerezani hapo pamoja na Mbowe ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu.

Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe.

 

Machi 28, mwaka huu, washtakiwa hao walifik­iswa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka hayo na kukosa dhamana.

Machi 29, mwaka huu wa­liruhusiwa kupata dhamana mahakamani hapo lakini ikashindikana baada ya mahakama kuelezwa kuwa gari lililokuwa likiwapeleka mahabusu hao mahakamani liliharibika hivyo viongozi hao kutopelekwa mahaka­mani na kubaki gerezani.

 

Ilielezwa pia, mawakili wa upande wa serikali waliieleza mahakama kuwa wameku­sudia kuweka pingamizi la dhamana hiyo Mahakama Kuu ya Tanzania.

Leo, viongozi hao wana­tarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuka­milisha taratibu za dhamana zao.

Stori: BONIFACE NGUMIJE NA NEEMA ADRIAN,DAR

Comments are closed.