The House of Favourite Newspapers

Paul Okoye Ampa Jina Mtoto Mgonjwa Hospitalini

0

paulcc MMOJA wa watoto wagonjwa katika hospitali ya Hearts of Gold Children Hospice iliyoko Surulere, Lagos, nchini Nigeria, ambayo inauguza watoto walio katika hali mbaya, Ijumaa iliyopita alipata bahati ya kupewa jina na mwanamuziki maarufu nchini humo, Paul Okoy wa kundi la P-Square.

pauloMwasisi wa kituo hicho cha tiba, Bi Laja Adedoyin, alisema kwamba mtoto huyo, Blessing Ngozi,  mwenye umri wa miezi minne alikuwa hajapata jina tangu alazwe hapo na yeye (Adedoyin) ndiye aliyetoa kibali cha kumpa jina ‘kadogoo’ huyo ambapo Paul alimpa jina la Blessing.

rude-boy-psquarePaul ambaye aliitembelea hospitali hiyo akiwa na watu wa familia yake, marafiki na wasanii kutoka kampuni yake ya kurekodi nyimbo ya Lucy and Muno, alitoa misaada ya chakula na vitu vingine.  Baada ya hapo aliendesha sala ya kumwombea kila mtoto katika kituo hicho na viongozi wao.

Leave A Reply