The House of Favourite Newspapers

Pawasa awafungia kazi Malawi Beach Soka

0

 

 

 

Kocha wa Timu ya Taifa ya soka la Ufukweni Boniface Pawasa

TIMU ya taifa ya Tanzania ya Ufukweni walipoteza dhidi ya Malawi ugenini kwa mabao 3-2 ambapo mchezo wa marejeano unatarajiwa kufanyika Agosti 8 katika uwanja wa fukwe za Coco,Dar.

Akizungumza, Pawasa alisema kuwa sababu kubwa ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini kutokana na uwanja kuwa sio sahihi kwa soka la ufukweni jambo ambalo anaamini katika mchezo wa marejeao watapata ushindi kwa kuwa uwanja wa nyumbani unaruhusu.

Timu ya Taifa ya Ufukweni inatarajiwa kucheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Malawi Agosti 8, 2020 kwenye fukwe za Coco.

“Tulipoteza dhidi ya Malawi kutokana na wao kuwa na uwanja ambao sio sahihi kwa soka la ufukweni jambo ambalo lilisababisha sisi kushindwa kucheza mchezo sahihi na wao wakawa wanacheza kama mpira wa kawaida wa miguu.

“Kwa kuwa tunakwenda kucheza katika Uwanja wetu wa nyumbani ambao ni mzuri kwaajili ya soka la ufukweni basi tunaamini tutacheza mchezo mzuri na kupata matokeo kisha kufuzu BAFCON,”alisema kocha huyo.

Leave A Reply