visa

PENNY, HABARI YA NDOA NITASHANGILIA WENZANGU TU, MIMI HAPANA!

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Harusi Yetu kupitia Runinga ya Magic Swahili, Penieli Mwingilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa anafurahi anapoona wenzake wakifunga na kutangaza ndoa zao lakini jambo hilo hataki litokee kwake.  Akizungumza na SHUSHA PUMZI, Penny alisema kuwa, moyo wake bado hauko tayari kuingia kwenye ndoa kwa sasa mpaka atakaporidhia hapo baadaye.

“Nafanya kipindi cha harusi, lakini huwezi amini napenda sana kuona watu wakioana na kuvaa mashela vile lakini mimi sipendi kabisa kuingia kwenye ndoa. Nafsi yangu inaona wazi bado haihitaji ndoa,” alisema Penny.
Toa comment