The House of Favourite Newspapers

Taasisi ya Doris Mollel Yatoa Msaada Bagamoyo

Misaada ikikabidhiwa kwa wananchi wa Bagamoyo.

 

TAASISI ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Shirika la Kiserkali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA) imetoa msaada  wa chakula kwa wananchi wasiojiweza katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya sadaka ya iftar kufuatia mwendelezo wa ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambao unaelekea ukingoni sasa.  Msaada huo ulihusisha mchele, mafuta, tende, n.k.

Wakati huohuo, Ubalozi wa Oman nchini umeshirikiana na Taasisi ya Doris Mollel katika kuwazawadia mavazi wananchi hao kwa maandalizi wa sikukuu ya Eid el Fitr, ambapo wamewapatia kanzu, vikoi na khanga kina mama.  Msaada huo umegusa kaya 250 za vijiji mbalimbali wilayani Bagamoyo vikiwemo Kitopeni, Mataya, Buma Madrasa, Ramiya na Makurunge.

 

Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa alishirikiana na Taasisi ya Doris Mollel katika kulifanikisha zoezi hilo kikamilifu.

 

 

 

 

Comments are closed.