The House of Favourite Newspapers

PENZI LA UWOYA LAMVURUGIA KALALA JUNIOR

 

Irene Uwoya

UBUYU mpya mjini ni kwamba mwanamama kiwango kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Irene Uwoya anamzimia usipime mkali wa miondoko ya Dansi, Kalala Hamza ‘Kalala Junior’ kiasi cha kumhonga vitu mbalimbali ili wawe pamoja. Baada ya kunasa tetesi hizo kutoka kwa chanzo cha kuaminika, Risasi Vibes ilimtafuta Kalala ili aweke wazi juu ya madai hayo ya kuhongwa na kuivuruga ndoa ya mwanamama huyo na Dogo Janja.

Alipopatikana Kalala alisema: “Ni kweli nimeyasikia hayo maneno. Hata kwenye mitandao nimeona, lakini si kweli kabisa na nikwambie tu, tangu yaanze kusemwa yananivurugia hata kwenye uhusiano wangu. “Nina mtu wangu ninampenda na sipo na Uwoya ingawa ni rafiki yangu na mtu ambaye tunafahamiana.”

Risasi Vibes ilimtafuta pia Uwoya ili aweze naye kufungukia madai hayo, lakini hakuweza kupatikana kwani alikuwa nje ya nchi (Dubai) hivyo jitihada zinaendelea. Kwa upande wake, Dogo Janja alipotafutwa na kupatikana hakutaka kuzungumza lolote juu ya ndoa yake.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.