The House of Favourite Newspapers

Penzi la Vanessa, Swahiba wa 50 Cent Gumzo

MJI umechafuka! Si mitandao kila kona habari ya mjini ni madai ya penzi jipya mjini kati ya mwanadada anayesumbua katika Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na mwanamuziki ambaye pia ni muigizaji swahiba wa rapa kutoka Marekani, Curtis James Jackson III ’50 Cent’, Olurotimi Akinosho ‘Rotimi’.

 

Kwa mujibu wa mtandao mkubwa wa habari za udaku, The Shed Room, wawili hao wapo kwenye uhusiano kwa muda mrefu na hivi karibuni walinaswa kwa mara ya kwanza wakila bata maeneo ya Miami nchini Marekani.

 

Mtandao huo ulianika kipande cha video kikimuonesha Rotimi mwenye asili ya nchini Nigeria akiwa pembeni ya bwawa la kuogelea akivuta shisha pembeni akimshika mikono huku sauti inayodaiwa ni ya Vee Money ikisikika.

 

Mbali na video hiyo, waliweka picha walizoposti mara ya mwisho wawili hao kwa nyakati tofauti kupitia kurasa zao za Instagram ambapo Vee Money aliweka akiwa amevaa mavazi ya ufukweni, akipuliza moshi wa shisha na kuandika eneo alipo kuwa ni South Beach, Miami, Florida na ndani ya lisaa limoja Rotimi naye aliweka picha katika ukurasa wake akiwa na pensi akipuliza shisha eneo hilohilo alilopo mrembo huyo.

 

Rotimi ni muigizaji, mwanamitindo, msanii wa muziki aliyesainiwa chini ya Lebo ya G Unit inayosimamiwa na 50 Cent. Kiasili baba yake ni mtu kutoka Yoruba nchini Nigeria wakati mama ni Igbo kutoka Nigeria.

 

Alianza kujulikana kwenye Tamthiliya ya Boss akicheza kama Darius Morrison. Kwa sasa anakubalika mno kupitia Tamthiliya ya Power ya 50 Cent akitumia jina la Andre Coleman ambapo mara kwa mara amekuwa akionekana na 50 Cent.

 

Kabla ya kunasa kwa Rotimi, Vee Money anayetikisa kwa sasa na Wimbo wa Bado akimshirikisha Rayvanny, alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na na msanii wa R&B, Juma Musa ‘Jux’ ambapo kapo yao iliyodumu kwa miaka tisa kisha kuvunjika huku sababu zikifichwa. Tangu kuachana kwa kapo hiyo, Jux alianzisha uhusiano wa kimapenzi na Nayika Thongom mwenye asili ya Thailand.

Stori: Andrew Carlos, Dar

Comments are closed.