The House of Favourite Newspapers

Phiri atuma salamu Simba, Yanga

0


MSHAMBULIAJI wa Zesco FC ya nchini Zambia, Moses Phiri ambaye Simba na Yanga zimekuwa zikionesha nia ya kumsajili kwenye usajili wa dirisha dogo, ametuma salamu baada ya wikiendi kufunga bao.

 

Phiri alifunga bao moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu Zambia dhidi ya Kabwe Warriors uliomalizika kwa Zesco kushinda mabao 2-1.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Phiri amesema kuwa: “Bao lile ni kama salamu kwa mashabiki wangu hasa wa Tanzania ambao muda sio mrefu huenda nikajiunga nao.”

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Leave A Reply