The House of Favourite Newspapers

Picco: Walinizushia Natumia Madawa, Wakazusha Tena Nimefungua Msikiti – Video

0

Msanii Picco aliyeimba Kikongwe akiwa studio za +255 Global RadioMsanii wa kitambo wa Bongo Fleva aliyejipatia umaarufu kwa wimbo wake wa Kikongwe akiwa na Kundi la SARS, Picco amesema katika maisha yake amekuwa akizushiwa mambo mbalimbali kwa lengo la kumpoteza kwenye ramani ya muziki.

Akifanya mahojiano katika Kipindi cha Mapito kinachorushwa na +255 Global Radio na Global TV, Picco anasema amewahi kuzushiwa kwamba anatumia madawa ya kulevya, baadaye wakamzushia tena kwamba ametopea kwenye ulevi wa kupindukia mambo ambayo hayana ukweli wowote.

Ameongeza pia kuwa kuna kipindi pia aliwahi kuzushiwa kwamba amefungua msikiti wake, jambo ambalo pia halikuwa na ukweli wowote na kusisitiza kwamba yupo timamu na anaendelea na shughuli zake nje ya muziki ambazo ndizo zinazomuwezesha kujikimu kimaisha.

 

Msanii Picco aliyeimba Kikongwe akiwa studio za +255 Global Radio

Leave A Reply