The House of Favourite Newspapers

PICHAZ: Shughuli ya Uokoaji kwa Waliofukiwa na Kifusi Pugu Inaendelea

SHUGHULI ya kuokoa miili ya watu wawili waliofukiwa na kifusi katika Machimbo ya kokoto ya Golani yaliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam bado inaendelea ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema pamoja na Kamanda ya Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salumu Hamduni ambapo mpaka sasa watu hao bado hawajapatikana.

Kwa mujibu wa DC  Mjema amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana Alhamisi majira ya saa 8 mchana ambapo ameeleza kuwa watu wanne walifukiwa na kifusi hicho ambapo mmoja alipatikana akiwa amefariki na mwingine majeruhi aliyevunjika mguu.

Mwili wa marehemu ulipekewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na majeruhi naye alipelekwa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa.

Shughuli ya uokoaji inaendelea ili kutafuta miili ya watu wawili kati ya wanne walifukiwa jana.

Aidha DC Mjema ameeleza kuwa eneop hilo lilishapigwa marufuku na serikali kuchimba mchanga ama kokoto licha ya wananchi kuamua kukaidi amri ya serikali na kendelea kuchimba.

Nimekuwekea picha za kutosha ushuhudie tukio hilo.

 

Story: Na Hilaly Daud

TAZAMA VIDEO DC MJEMA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.