The House of Favourite Newspapers

Pigo Moja Simba Chali Taifa, Cannavaro Nikipangwa Wameisha

KOCHA wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema hana wasiwasi na mechi ya leo dhidi ya Simba kwani anakiamini kikosi chake ambacho anasema kitatoa dozi kwa wapinzani wao.

Jeuri hiyo ya Pluijm, raia wa Uholanzi, imekuja kutokana na dozi aliyoitoa kwa wachezaji wake walipokuwa kambini Pemba kabla ya kurejea Dar es Salaam jana jioni kwa ndege. Saa 10:00 jioni ya leo, Yanga itacheza na Simba mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini Pluijm ametamba kuimaliza tena Simba. Msimu uliopita, Pluijm aliifunga Simba mara mbili kwa mabao 2-0 kila mechi.

yanga2

Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia.

Akizungumzia mchezo huo, Pluijm alisema: “Tumejiandaa vizuri, kila kitu kipo sawa, vijana wapo tayari kiakili na kisaikolojia kwa ajili ya mchezo wenyewe. “Tutawapiga pigo takatifu kama mechi zilizopita, hata hivyo najua mchezo utakuwa mgumu sana lakini baada ya dakika 90, tuna imani kubwa ya kuibuka washindi.”
Yanga vs African Lyon (2)

Kikosi cha timu ya Yanga.

Pluijm alisema anataka ushindi ili kupunguza tofauti ya pointi kati yao na Simba kwani wapinzani wao wapo kileleni na pointi 16 wakati wao wapo nafasi ya tatu na pointi 10. “Tunataka kushinda ili kupunguza tofauti ya pointi ndiyo maana mchezo huu ni muhimu kwetu, naamini tutashinda,” alisema Pluijm.

BUSUNGU, MWASHIUYA WAZINGUA
Leo Yanga itamkosa mshambuliaji wake Malimi Busungu na kiungo mshambuliaji Geoffrey Mwashiuya ambao ni majeruhi. Mwashiuya anaumwa goti.

yanga-simba-copy

Wachezaji wa timu ya Yanga wakipambana na wa Simba katika mechi iliyopita.

“Mwashiuya na Busungu ndio hawapo fiti asilimia zote kufikia leo (jana Ijumaa), wameshaanza mazoezi lakini ukweli hawapo fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho (leo),” alisema Pluijm.

CANNAVARO AKIPANGWA KAZI MNAYO
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akizungumzia mchezo huo, alisema: “Kama nikipangwa nakuhakikishia Simba watakiona cha moto, waombe nisipangwe tu.”

1.Ali Mustapha ‘Barthez’

2. Juma Abdul

3.Hajji Mwinyi

4.Andrew Vicent

5.Vincent Bossou

6.Mbuyu Twite

7.Simon Msuva

8.Thaban Kamusoko

9.Donald Ngoma

10.Amissi Tambwe

11.Deus Kaseke YANGA SC:

AKIBA: 1.Deogratius Munishi ‘Dida’ 2.Hassani Kessy 3.Oscar Joshua 4.Kelvin Yondani 5.Nadir Haroub ‘Cannavaro’ 6.Haruna Niyonzima 7.Juma Mahadhi

Comments are closed.