The House of Favourite Newspapers

Pistorius Akimbizwa Hospitali

0

Oscar-Pistorius

Oscar Pistorious.

Na Leonard Msigwa/Mtandao

MWANARIADHA mlemavu aliyehukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani huko nchini Afrika Kusini kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Oscar Pistorious amekimbizwa hospitali ya Pretoria Kalafong baada ya kuanguka kitandani na kuumia.

Reeva-Steenkamp

Reeva Steenkamp.

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake, lakini kwa sasa amerejeshwa gerezani.

Kumeibuka uvumi katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini kuwa Pistorius alikuwa amejaribu kujitia kitanzi lakini hilo limekanushwa na familia ya mwanariadha huyo.

GettyImages-457596782

Gereza alipofungwa Pistorius.

Mwanariadha huyo alimuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi nyumbani kwake katika Siku ya wapendanao (Valentine’s Day) mwaka wa 2013, akisema kuwa alidhania ni mwizi.

 

Profesor Jay “Mazuri na Mabaya ya Serikali ya Magufuli Niliyoyaona ni Haya Hapa’

Leave A Reply