The House of Favourite Newspapers

Pluijm: Yanga Tunawajua, Hawatusumbui

Mholanzi Hans van Der Pluijm akiongea na wachezaji wake.

KOCHA wa timu ya Singida United, Mholanzi Hans van Der Pluijm kuele­kea kwenye mechi yao ya leo Jumatano dhidi ya Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, amefunguka kuwa watatu­mia mbinu ya Manchester United kuwamaliza wapin­zani wao.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema wameshacheza na Yanga mara tatu hivyo wanajua udhaifu wa wapinzani wao upo wapi na kama waliweza kuwafunga katika uwanja wao basi hata Dar wanaweza kuwafunga.

Kikosi cha timu ya Yanga.

“Tumeshacheza nao mara tatu na hawa mabingwa wa­tetezi hivyo siwezi kuzungumza sana kwani tuna mechi kubwa na ngumu, hii ni nafasi nzuri ya wachezaji kuonyesha uwezo wao wenyewe na kitu gani wanakitaka baadaye, tunatak­iwa tupambane kwa nidhamu juhudi na kwa umoja zaidi.

 

“Kule Singida ilionyesha kwamba inawezekana ku­wafunga lakini sasa ipo juu ya wachezaji kufanya kweli, tu­meona kitu walichofanya Man­chester United walipocheza na Man City, hivyo sisi tunataka kuchukua mfano ule walio­fanya kwenye kipindi cha pili wa kuonyesha juhudi na kushinda, kwenye mpira kila kitu kinawezekana na hakuna kisichowezekana,” alisema Pluijm.

Stori: Ibrahim Mressy

Comments are closed.