The House of Favourite Newspapers

Pogba: Liver Game Ngumu Kuliko Man City

pogbaKIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba, amesema kuivaa Liverpool ni mchezo mkubwa zaidi kwa klabu yake kuliko hata ule dhidi ya Manchester City.

United jana walivaana na Liverpool kwenye Uwanja wa Old Trafford, wakijua kwamba ushindi ungekata pengo la pointi baina yao na Liver hadi kuwa tofauti ya pointi mbili. “Historia ya Liverpool vs Man United – ni gemu kubwa, nadhani zaidi hata ya Man City, kwa sababu ya yale mazingira unayojisikia,” alisema Pogba, 23.

Pogba alicheza katika mechi ya kwanza dhidi ya Liver Anfield iliyoisha kwa suluhu.

Comments are closed.