The House of Favourite Newspapers

Pointi Tisa Zamtisha Aussems

simbaBOSI mkuu wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amefunguka kuwa kichwa kinamchemka kutokana na dakika 270 ambazo ziko mbele yake kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Kocha huyo amesema hayo kutokana na ratiba ya Simba ambapo leo Jumatano watakuwa na mechi dhidi ya Azam FC, kisha Jumapili watacheza na Singida United mkoani Arusha kisha watasafiri kuelekea Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

 

Aussems ameliambia Championi Jumatano, kuwa hiyo ni ratiba ngumu kwao kutokana na kucheza kwa karibu karibu lakini anaendelea kujiandaa kuona wanashinda kwenye mechi zote.

 

“Tuna mechi tatu zijazo za ligi ambapo tutaanza kucheza na Azam FC kesho (leo) Jumatano, ambapo huu ni mchezo muhimu kwetu.

 

“Lakini pia tutakuwa na mechi dhidi ya Singida United na Mwadui FC. Mechi zote hizi zipo karibu zikiwa zinapishana kwa siku chache kila tutakapomaliza mechi moja, lakini hakuna namna zaidi ya kucheza.

 

“Kitu cha kwanza ni kuanza na mechi yetu ya kwanza kabisa dhidi ya Azam ambayo ndiyo ninaendelea kuifikiria namna gani nipate ushindi lakini pia kwenye mechi nyingine ambazo zitakuwa zimebaki nataka kuona tukishinda kwa ajili ya kujiongezea pointi tukiwa kileleni,” alisema Aussems.

Comments are closed.