The House of Favourite Newspapers

Polisi Dar  wakabidhiwa Tani 60 za saruji

Lori lililokuwa limepakia suruji hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.

 

 

POLISI Mkoa wa Dar es Salaam wamekabidhiwa Tani 60 za mifuko ya Saruji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo Juni 24 mwaka huu ambapo ametimiza ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni.

 

Saruji hiyo ni sawa na mifuko 1,200 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 kwa askari bora 12 waliochaguliwa hivi karibuni na Jeshi la Polisi kutokana na utendaji kazi mzuri.

 

Akikabidhi saruji hiyo, Makonda amesema lengo la kutoa zawadi hiyo ni kujenga morali ya kazi kwa askari wanaojitoa kwa hali na mali kulinda usalama wa raia na mali zao jambo linalopelekea Dar es Salaam kuwa salama.

 

Mifuko hiyo ya Saruji imetolewa na Kampuni ya Nabis Cooperate Ltd iliyounga mkono jitihada za Makonda katika kugusa maisha ya Wananchi katika masuala mbalimbali.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabis Cooperate Ltd Mhandisi, Thomas Wiso amesema kuwa wameamua kutoa saruji hiyo kuunga mkono jitiada za Makonda kujali wananchi wake na kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwa Shwari.

Comments are closed.