The House of Favourite Newspapers

Polisi Mbaroni kwa Kushambulia Waandamanaji Nigeria

0

MAMLAKA mjini Lagos, Nigeria, imewakamata polisi waliowashambulia waandamanaji wanaoendelea kuandamana dhidi ya ukatili wa polisi.

 

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa polisi walifyatua risasi katika kundi la waandamanaji katika eneo la Surulere mjini humo.

 

Gavana wa jimbo la Lagos, Babajide Sanwo-Olu, aliwataja majina polisi hao wanne ambao amesema wanakabiliwa na kesi inayohusu nidhamu.

 

Amesema kwamba jimbo limetenga naira milioni 200 (dola 521,000) kwa ajili ya kufidia waathiriwa wa ukatili wa polisi.

 

Serikali ya shirikisho imepiga marufuku maandamano katika mji mkuu ili kutekeleza maadili ya kukabiliana na Covid-19. Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yamefanyika katika miji yote nchini Nigeria katika kipindi cha wiki iliyopita.

 

Maandamano yameendelea licha ya kuvunjwa kwa kikosi tata cha polisi kinachotuhumiwa kwa ukatili dhidi ya  raia,  maarufu kama Sars.

Leave A Reply