The House of Favourite Newspapers

Polisi Ahukumiwa Adhabu ya Kifo kwa Mauaji ya Wakili nchini Kenya

0

Mahakama nchini Kenya imemhukumu adhabu ya kifo polisi kwa mauaji ya wakili maarufu wa masuala ya haki za binadamu na wengine wawili miaka zaidi ya sita iliyopita.

Polisi wengine wawili wa zamani na raia wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 na 39 jela kwa mauaji ya wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi waliouawa mwezi Juni mwaka 2016.

Polisi watatu na raia walipatikana na hatia kwa mauaji ya wakili wa masuala ya haki za binadamu Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi.

Wanne hao,Fredrick Leliman, Stephen Cheburet, Sylvia Wanjiku na Peter Ngugi, walipatikana na hatia ya mauaji ya Bw kimani, mteja wake Josephat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri.

Mke wa marehemu wakili na familia yake walikuwepo mahakamani wakati hukumu hiyo ilipotangazwa katika mahakama, mjini Nairobi.

Miili ya Bw Kimani na watu wengine wawili ilipatikana baada ya kutupwa mtoni viungani mwa mji mkuu , Nairobi.

Wakili Kimani alikuwa akimtetea Mwendwa, ambaye ni dereva wa pikipiki ambaye alikuwa anamshutumu Bw Leliman – mmoja wa maafisa watatu wa polisi waliopatikana na hatia – kwa kumpiga risasi bila sababu katika kituo cha ukaguzi wa magari mnamo mwaka 2015.

Bw Kimani, Bw Mwendwa na Bw Muiruri walionekana kwa mara ya mwisho tarehe 23 Juni 26 kwenye kituo cha polisi.

Miili yao iliyokatwa iligundulika wiki mbili baadaye katika mto uliopo takriban kilomita 100(maili 62) kutoka mji mkuu.

Hukumu hii inakuja wakati huduma ya polisi nchini Kenya ikichunguzwa zaidi kuhusiana na mauaji ya kiholela na utekaji nyara.

Rais William Ruto tayari amevunja vikosi kadhaa maalum vya polisi vinavyoshutumiwa kwa mauaji na utekeji wa raia.

EXCLUSIVE: KUMBE SCORPION ALIYEMTOBOA MACHO SAID SIYE ALIYEFUNGWA? SAMJET ATOKA GEREZANI, AFUNGUKA

Leave A Reply