The House of Favourite Newspapers

POLISI WAFANYA UPEKUZI NYUMBANI KWA ZITTO KABWE

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni limefanya upekuzi nyumbani kwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Novemba 1, 2018.

Zitto ambaye alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwake na kupeleka katika Kituo cha Polisi Oysterbay ambako alihojiwa kisha kuhamishiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Wakili wake, Jebra Kambole amethibitisha polisi kupekuwa nyumbani kwa Zitto na kusema baada ya mteja wake kupelekwa Sentro, alihamishiwa kituo kingine kilichopo Mburahati ambako ndiko alilala na leo asubuhi alirudishwa tena Kituo cha Polisi Oysterbay.

 

“Leo asubuhi mteja wangu aliongozana na polisi hadi nyumbani kwake Masaki ambako wamefanya upekuzi kisha akarudishwa kwenye Kituo cha Oysterbay, bado tunashughulikia suala la dhamana yake, lakini sina uhakika iwapo watampa dhamana leo,” amesema Kambole.

Comments are closed.